9/18/2020

TANROADS: UJENZI WA DARAJA LA SIBITI WAKAMILIKA KWA ASILIMIA 100

 

Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini  (TANROAD) Mkoa wa Singida,  Mhandisi  Matari Masige (kulia) akitoa taarifa fupi ya kazi ya ujenzi wa daraja la Sibiti ambalo linaunganisha Mkoa wa Singida na Simiyu kwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)  na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi. 
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)  na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (katikati) akikagua daraja hilo.
Muonekano wa daraja hilo.
Wananchi wa Kata ya Bukumbi Wilayani Meatu mkoani Simiyu wakipita kwenye daraja hilo.
Kazi za ujenzi zikiendele katika daraja hilo.

Dotto Mwaibale na Ismail Luhamba, Singida

 Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini  (TANROAD) Mkoa wa Singida,  Mhandisi  Matari Masige amesema kazi ya ujenzi wa daraja la Sibiti ambalo linaunganisha Mkoa wa Singida na Simiyu imekamilika kwa asilimia 100.

Masige aliyasema hayo jana kwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)  na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati  aliposimama kwenye daraja hilo akiwa kwenye ziara yake ya kampeni ya kumuombea kura Mgombea urais wa chama hicho Dkt. John Magufuli, wabunge na madiwani akitokea wilayani Mkalama mkoani Singida akielekea mkoani Simiyu ambapo alijionea ujenzi wake na kupata maelezo mafupi na kuliridhishwa na kazi hiyo.

"Mhe.Waziri Mkuu kazi ya ujenzi wa daraja ili imekamilika tunacho kifanya hivi sasa ni matengenezo madogo madogo na njia ya kupitisha mifugo ambazo zinajengwa chini ya daraja na kuiwezesha mifugo kwenda upande wa pili kunywa maji pasipo kupita juu ya daraja." alisema Masige.

Masige alisema kukamilika kwa ujenzi wa  daraja hilo kutawapunguzia adha ya usafiri wananchi wa kanda ya kati na kanda ya ziwa.

Alisema barabara hiyo itapunguza zaidi ya kilometa 200 ambazo zilikuwa zikitumika kutoka Singida mpaka Musoma kwa kupitia Nzega, Shinyanga, Mwanza ambapo Musoma ni kilometa 720 lakini kwa kupitia njia ya Singida, Simiyu mpaka Musoma itakuwa ni kilometa 520 hivyo watakuwa wamepunguza kilometa hizo.

Mhandisi Masige alimuahidi Waziri Mkuu Majaliwa na kumhakikishia kuwa daraja hilo litakamilika kwa wakati na kwa viwango  vinavyohitajika. 

Waziri Mkuu Majaliwa baada ya kupokea taarifa hiyo fupi ya kazi ya ujenzi wa daraja hilo alisema Serikali imemaliza kuunganisha mikoa kwa barabara za lami na sasa inakwenda kuunganisha barabara za wilaya kwa wilaya kwa lami na kusaidia  kukuza uchumi wa wananchi na Taifa kwa ujumla.

Alisema Mkandarasi anaye jenga barabara hiyo kama atamaliza kazi kwa wakati Serika itamuongeza kipande kingine cha kutoka Meatu hadi Iguguno hivyo alimsihi kufanya kazi hiyo kwa weledi na kwa viwango vinavyohitajika.

Daraja hilo lina urefu wa mita 82, nguzo tatu zenye kimo cha mita saba kila moja huku tuta la barabara likiwa na mita 11 na makaravati 66 na limeghalimu zaidi ya sh. billioni 20.

    

0 comments:

Post a Comment