Posts

MAJALIWA AZINDUA KAMPENI ZA CCM MKOA MANYARA

Image
Waziri Mkuu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Kassim Majaliwa  akizungumza wakati alipozindua Kampeni za CCM Mkoa wa Manyara kwenye uwanja wa Kwaraa mjini Babati, Septemba 1, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wakati alipowasili kwenye uwanja wa Kwaraa mjini Babati kuzindua Kampeni za CCM Mkoa wa Manyara, Septemba 1, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu na Mjumbe wa Kamati ya CCM Taifa, Kassim Majaliwa  akimkabidhi nakala ya Ilani ya Uchaguzi, Mgombea Ubunge wa CCM wa Jimbo la Babati Mjini, Pauline Gekul, baada ya kuzindua Kampeni za CCM Mkoa wa Manyara  kwenye uwanja wa Kwaraa mjini Babati, Septemba 1, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)   

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMATANO SEPTEMBA 2, 2020

Image
 

WAHANDISI 264 WACHUKULIWA HATUA KUKIUKA MAADILI

Image
NA MWANDISHI WETU, DODOMA BODI ya Usajili wa Wahandisi (ERB), imesema kuwa imechukua hatua kwa wahandisi 264 katika kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2015 hadi 2020 kutokana na makosa mbalimbali ya ukiukwaji wa maadili ya taaluma ya kiuhandisi ambayo ni kinyume na kiapo chao. Hayo yamesemwa na Msajili wa Bodi hiyo Mhandisi Patrick Barozi, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, kuhusiana na maadhimisho ya Siku ya Wahandisi kwa mwaka huu ambayo yatafanyika jijini humo tarehe 3 na 4 mwezi Septemba. Mhandisi Barozi, amefafanua kuwa hatua hiyo huchukuliwa na bodi hiyo  mara tu baada ya wahandisi hao kula kiapo cha utii ambacho kinawakumbusha kuwajibika vyema kwenye taaluma zao na maamuzi yao ya utendaji wao wa kihandisi wa kila siku. “Bodi imechukua hatua mbalimbali  kwa wahandisi 264 ikwemo kuwaonya na kuwapeleka mahakamani wahandisi ambao walionekana kukiuka kiapo chao cha utii katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, na itaendelea kufuatilia wahandisi amb

WAZIRI HASUNGA AZINDUA MATREKTA 7 NA ZANA ZAKE ILI KUONGEZA UZALISHAJI WA MBEGU NA MICHE BORA YA MAZAO

Image
  Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga akisisitiza jambo  wakati wa uzinduzi wa Matrekta na zana zake ili kuimarisha uzalishaji wa mbegu uliofanyika katika Taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania (TARI)  eneo la Makutupora Jijini Dodoma   leo tarehe 1 Septemba 2020 . (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo) Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga akisisitiza jambo  wakati wa uzinduzi wa Matrekta na zana zake ili kuimarisha uzalishaji wa mbegu uliofanyika katika Taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania (TARI)  eneo la Makutupora Jijini Dodoma   leo tarehe 1 Septemba 2020 .  Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Hunges Motors Tanzanaia Ndg Alex Duffar akitoa maelezo ya kina kuhusu matrekta New Holanda mbele ya Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga mara baada ya k uzindu a  Matrekta saba na zana zake ili kuimarisha uzalishaji wa mbegu uliofanyika katika Taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania (TARI)  eneo la Makutupora Jijini Dodoma   leo tarehe 1 Septemba 2020 . Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga  akimsikiliza M

BILIONI 12 ZA WAKULIMA WA KAHAWA KULIPWA KESHO

Image
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya (kushoto) akiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Prof.Riziki Shemdoe (kulia) wakati wa kikao kilichojadili ulipwaji wa madeni ya wakulima wa zao la kahawa kwa vyama vikuu vya ushirika KDCU na KCU utakaonza kesho .Kikao kimefanyika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza .  Picha ya pamoja kati ya Makatibu Wakuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya ( wa pili kushoto)  akiwa kwenye kikao leo Mwanza kujadili kuanza kulipwa kwa wakulima wa Kahawa Kagera.Wengine ni Bw.Emanuel Tutupa (RAS Mwanza) katikati,Prof.Riziki Shemdoe ( Katibu Mkuu Viwanda) na Prof.Faustin Kamuzola (RAS Kagera aliyevaa kofia).  Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya (katikati) akiongea na waandishi wa habari leo jijini Mwanza kutangaza uamuzi wa kuanza kuwalipa wakulima wa kahawa wa mkoa wa Kagera fedha zao shilingi Bilioni 12 kupitia Vyama Vikuu vya KDCU na KCU.Kulia kwake ni Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Prof.Riziki Shemdoe. Katibu Mkuu Wizara ya Kili

MAELFU YA WANANCHI WAKIMSIKILIZA MWENYEKTI WA CCM RAIS DKT MAGUFULI AKIHUTUBIA MKUTANO WA HADHARA WA KAMPENI UWANJA WA BOMBADIER, SINGIDA

Image
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Rais Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia maelfu ya wananchi katika  mkutano wa hadhara wa kampeni Uwanja wa Bombadier mjini Singida leo Jumanne Septemba 1, 2020

MGOMBEA URAIS WA TANZANIA KUPITIA CCM, RAIS MAGUFULI AHUTUBIA IKUNGI

Image
Mgombea kiti cha Rais wa Tanzania kupitia CCM, Rais John Magufuli amehutubia mamia ya Wananchi wilayani Ikungi akiwa njiani kwenda Singida ambako Alasiri  hii ya Septemba 1, 2020 anatarajiwa kuhutubia mkutaano mkubwa wa kampeni. Uchaguzi Mkuu unatarajiwa kufanyika Oktoba 28, 2020 ambapo jumla ya vyama 15 vitachuana kuwania nafasi hiyo ya juu kabisa ya uongozi wa Nchi.