BILIONI 12 ZA WAKULIMA WA KAHAWA KULIPWA KESHO
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya (kushoto) akiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Prof.Riziki Shemdoe (kulia) wakati wa kikao kilichojadili ulipwaji wa madeni ya wakulima wa zao la kahawa kwa vyama vikuu vya ushirika KDCU na KCU utakaonza kesho .Kikao kimefanyika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza .
Picha ya pamoja kati ya
Makatibu Wakuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya ( wa pili kushoto) akiwa
kwenye kikao leo Mwanza kujadili kuanza kulipwa kwa wakulima wa Kahawa
Kagera.Wengine ni Bw.Emanuel Tutupa (RAS Mwanza) katikati,Prof.Riziki Shemdoe (
Katibu Mkuu Viwanda) na Prof.Faustin Kamuzola (RAS Kagera aliyevaa kofia).
Katibu Mkuu Wizara ya
Kilimo Bw.Gerald Kusaya (katikati) akiongea na waandishi wa habari leo jijini
Mwanza kutangaza uamuzi wa kuanza kuwalipa wakulima wa kahawa wa mkoa wa Kagera
fedha zao shilingi Bilioni 12 kupitia Vyama Vikuu vya KDCU na KCU.Kulia kwake
ni Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Prof.Riziki Shemdoe.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya (pichani) leo
ametangaza kuanza kulipwa kwa shilingi Bilioni 12 za wakulima wa kahawa mkoa wa
Kagera kupitia Vyama vikuu vya Ushirika KDCU na KCU.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza
Mhe.John Mongella ( katikati) akiongea na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo
Bw.Gerald Kusaya (kushoto) na Katibu Mkuu Viwanda na Biashara Prof.Riziki
Shemdoe (kulia) leo wakati wa kikao cha kujadili ulipwaji wa madeni ya wakulima
wa kahawa mkoa wa Kagera kilichofanyika Mwanza na kuhusisha viongozi wakuu wa
Vyama vya Ushirika KDCU na KCU.
Comments
Post a Comment