TANZANIA YAWA KITOVU CHA UWEKEZAJI NA UKUAJI UCHUMI NCHI KUSINI MWA JANGWA LA SAHARA
* Mfumuko wa bei wadhibitiwa, Neema yaja kwa wafanyabiashara wadogo MATOKEO Mazuri yaliyotokana na jitihada za Serikali kwa kuweka mazingira bora ya uwekezaji na ufanyaji biashara zimeiweka Tanzania kuwa kitovu cha uwekezaji na kupelekea ukuaji wa uchumi katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara kutoka asilimia 4.7 mwaka 2022 hadi kufikia asilimia 5.0 mwaka 2023 huku matarajio ya ukuaji uchumi kwa mwaka 2024 yakiwa asilimia 5.5. Hayo yameeelezwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango alipomwakilishwa Rais Samia Suluhu Hassan katika Jukwaa la Uwekezaji na Kodi 2024 lililofanyika Leo katika kituo cha mikutano cha kimataifa ya Julius Nyerere jijini Dar es Salaam na kueleza kuwa Serikali imeendelea kufanya maboresho ya sera na kanuni ili kujibu changamoto za uwekezaji na wafanyabiashara ili waweze kulipa kodi kwa hiari na kuiwezesha Serikali kutekeleza mahitaji kwa Umma. Mpango amesema kuwa, Jitihada hizo za Serikali ambayo imekuwa ikishirikiana na sekta