Posts

KUTOKA MAGAZETINI DESEMBA 29, 2023

Image
 

RAIS SAMIA ATUNUKIWA SHAHADA YA HESHIMA YA UZAMIVU

Image
Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Viongozi pamoja na wageni mbalimbali mara baada ya kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Uzamivu na Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kwa kutambua mchango wake wa kuifungua nchi kiuchumi kupitia Sekta ya Utalii kwenye Hafla ya Mahafali ya 19 ya Chuo hicho yaliyofanyika katika Ukumbi wa Dkt. Ali Mohamed Shein Kampasi ya Tunguu tarehe 28 Desemba, 2023 Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, akitunukiwa Shahada ya Heshima ya Uzamivu na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Viongozi wengine akiwa kwenye maandamano ya Kitaaluma wakati walipokuwa wakiingia kwenye Ukumbi wa Dkt. Ali Mohamed Shein Kampasi ya Tunguu kwa ajili ya kushiriki Hafla ya Mahafali ya 19 ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) ambapo Chuo hicho kimemtunuku Shahada ya Heshima ya Uzamivu kwa kutambua mchango

WAGANGA WAFAWIDHI RRH-TEMEKE, AMANA, MWANANYAMALA NA IRINGA WAWAFAGILIA WAUGUZI MUHIMBILI

Image
Waganga Wafawidhi wa Hospitali za Rufaa za Mikoa ya Temeke, Amana, Mwananyamala na Iringa wamewapongeza watoa huduma wa Hospitali ya Taifa Muhimbili hasa Wauguzi kutokana na huduma nzuri wanazotoa kwa wananchi wanaolazwa katika wodi mbalimbali. Hayo yamesemwa leo na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa, Dkt. Alfred Mwakalebela ambaye amelazwa Hospitalini hapa wakati akiwaelezea jinsi anavyoendelea vizuri na matibabu Waganga Wafawidhi wenzake Dkt. Bryceson Kiwelu (RRH-Amana), Dkt. Joseph Kimaro (RRH-Temeke), Muuguzi Mfawidhi (RRH-Temeke) Bi. Nuswe Ambokile pamoja na Dkt. Zavery Benela kutoka (RRH-Mwananyamala). Dkt. Mwakalebela amewaambia wenzake kuwa tangu amefika hospitalini hapa amehudumiwa vizuri kila mahali alipopita kuanzia idara ya magonjwa ya dharura, kwenye vipimo vya maabara na radiolojia na kuongeza kuwa amefanyiwa vipimo vingi na kupata majibu yake ndani ya muda mfupi. “Nimekaa hapa nimejifunza mengi hasa kutoka kwa wauguzi, naulizwa na kuelekezwa vizuri k

ZAIDI YA TANI 3 ZA DAWA ZA KULEVYA ZANASWA, WATU SABA WATIWA MBARONI

Image
NA K-VIS, BLOG, DAR ES SALAAM MADAWA ya kulevya zaidi ya tani 3 yamekamatwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini( DCEA) katika operesheni iliyoendeshwa Dar Es Salaam na Iringa. Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo amesema kiasi hicho cha dawa za kulevya kinajumuisha kilogramu 2,180.29 za dawa hatari aina ya methamphetamine na kilogramu 1001.71 aina ya heroin na kufanya kiasi kilichokamatwa kufikia kilogramu 3,182, sawa na tani 3.1. Amesema dawa hizo zilikamatwa katika operesheni ya siku 18 kuanzia Desemba 5 hadi Desemba 23, 2023 na ilitekelezwa katika wilaya ya Kigamboni, Ubungo na Kinondoni Jijini Dar es Salaam pamoja na Wilaya ya Iringa mkoani Iringa. Kamishna Jenerali Lyimo amesema, watu saba (7) wawili kati yao wana asili ya Asia wamekamatwa kuhusiana na “mzigo” huo ambao   Mkuu huyo wa DCEA, ameuelezea kuwa ni kiasi kikubwa kuwahi kukamatwa katika historia ya nchi yetu “ Endapo dawa h

KUTOKA MAGAZETINI DESEMBA 28, 2023

Image