RAIS SAMIA ATUNUKIWA SHAHADA YA HESHIMA YA UZAMIVU

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Viongozi pamoja na wageni mbalimbali mara baada ya kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Uzamivu na Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kwa kutambua mchango wake wa kuifungua nchi kiuchumi kupitia Sekta ya Utalii kwenye Hafla ya Mahafali ya 19 ya Chuo hicho yaliyofanyika katika Ukumbi wa Dkt. Ali Mohamed Shein Kampasi ya Tunguu tarehe 28 Desemba, 2023
Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, akitunukiwa Shahada ya Heshima ya Uzamivu na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Viongozi wengine akiwa kwenye maandamano ya Kitaaluma wakati walipokuwa wakiingia kwenye Ukumbi wa Dkt. Ali Mohamed Shein Kampasi ya Tunguu kwa ajili ya kushiriki Hafla ya Mahafali ya 19 ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) ambapo Chuo hicho kimemtunuku Shahada ya Heshima ya Uzamivu kwa kutambua mchango wake wa kuifungua nchi kiuchumi kupitia Sekta ya Utalii tarehe 28 Desemba, 2023.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Viongozi pamoja na wageni mbalimbali mara baada ya kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Uzamivu na Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kwa kutambua mchango wake wa kuifungua nchi kiuchumi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Rais Mstaafu wa Zanzibar Mhe. Dkt. Aman Abeid Karume katika Ukumbi wa Dkt. Ali Mohamed Shein Kampasi ya Tunguu walipohudhuria Hafla ya Mahafali ya 19 ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) tarehe 28 Desemba, 2023.
Wahitimu katika ngazi mbalimbali wakiwa kwenye Hafla ya Mahafali ya 19 ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) yaliyofanyika katika Ukumbi wa Dkt. Ali Mohamed Shein Kampasi ya Tunguu tarehe 28 Desemba, 2023.

Comments

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"