ZAIDI YA TANI 3 ZA DAWA ZA KULEVYA ZANASWA, WATU SABA WATIWA MBARONI
NA
K-VIS, BLOG, DAR ES SALAAM
MADAWA
ya kulevya zaidi ya tani 3 yamekamatwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na
Dawa za Kulevya nchini( DCEA) katika operesheni iliyoendeshwa Dar Es Salaam na
Iringa.
Akizungumza
na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas
Lyimo amesema kiasi hicho cha dawa za kulevya kinajumuisha kilogramu 2,180.29
za dawa hatari aina ya methamphetamine na kilogramu 1001.71 aina ya heroin na
kufanya kiasi kilichokamatwa kufikia kilogramu 3,182, sawa na tani 3.1.
Amesema
dawa hizo zilikamatwa katika operesheni ya siku 18 kuanzia Desemba 5 hadi
Desemba 23, 2023 na ilitekelezwa katika wilaya ya Kigamboni, Ubungo na
Kinondoni Jijini Dar es Salaam pamoja na Wilaya ya Iringa mkoani Iringa.
Kamishna
Jenerali Lyimo amesema, watu saba (7) wawili kati yao wana asili ya Asia
wamekamatwa kuhusiana na “mzigo” huo ambao Mkuu huyo wa DCEA, ameuelezea kuwa ni kiasi kikubwa
kuwahi kukamatwa katika historia ya nchi yetu
“ Endapo dawa hizi zingefanikiwa kuingia mtaani zingeweza kuathiri zaidi ya watu milioni 76 kwa siku, na watuhumiwa waliokamatwa ni miongoni mwa mitandao mikubwa kabisa ya wauzaji wa dawa za kulevya, inayofuatiliwa nchini na duniani.”Amefafanua.
Comments
Post a Comment