Posts

GPE AND CAMFED HOST ROUNDTABLE ON EDUCATION WITH TANZANIAN CSOS

Image
Dar es Salaam, 29 th November 2023 - The Chair of the Board of Directors of the Global Partnership for Education (GPE), H.E. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, Retired President of the United Republic of Tanzania, along with GPE’s Chief Executive Officer, Ms. Laura Frigenti, are set to participate in a significant roundtable discussion today at the Campaign for Female Education (CAMFED) Tanzania offices in Dar es Salaam. According to Ms. Anna Sawaki, CAMFED Tanzania’s Director of Programs and Partnership, the primary objective of the roundtable is to collectively emphasise the importance of prioritising education on the political agenda. Additionally, she said, the event aims to recognise the pivotal role of Civil Society Organisations (CSOs) in advocating for education and actively contributing to policy dialogue within local education groups. “The roundtable will also provide an opportunity for CSO representatives to share their successful practices and experiences in supporting the t

FAO LA HUDUMA YA UTENGEMAO KUONGEZA FARAJA: PROFESA NDALICHAKO

Image
  NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID SERIKALI kupitia Mfuko wa Fidia kwa Wafanmyakazi (WCF) imetangaza Fao jipya la Huduma ya Utengemao wa Kijamii (Social Rehabilitation) kwa wafanyakazi wanaopata ulemavu na magonjwa yatokanayo na kazi na hivyo litawaongezea faraja, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Profesa Joyce Ndalichako, amesema. Akizungumza jijini Dar es Salaam,  Novemba 29, 2023, alipokutana na wanufaika wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu Duniani inayotarajiwa kufanyika kitaifa jijini Dodoma, Desemba 2, 2023, amesema  “Ndugu zangu hivi karibuni tutaanza kutoa Fao la Huduma ya Utengamao wa Kijamii na kutoa mafunzo ya kujenga ujuzi kwa wafanyakazi wanaopata ulemavu wakiwa kazini na aina ya ujuzi tutakaotoa utategemea uhitaji.” Alisema Alisema lengo la Serikali ni kumpatia mfanyakazi ujuzi ambao utaendana na hali ya ulemavu wake, mfano alikuwa dereva na akapata ajali il

KUTOKA MAGAZETINI NOVEMBA 29, 2023

Image
 

WALIOFARIKI KUONDOLEWA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA.

Image
  Mkurugenzi wa Habari na Elimu ya Mpiga Kura kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bi. Giveness Aswile akijadili jambo na Lazarus  Madembwe Mkuu wa TEHAMA Tume ya Taifa ya Uchaguzi  wakati akikagua vifaa katika zoezi la uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura kwenye kituo cha Masempele kata ya Ng'ambo mkoani Tabora leo Novemba 28,2023. Mkurugenzi wa Habari na Elimu ya Mpiga Kura kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bi. Giveness Aswile akisalimiana na Mkurugenzi wa Daftari na Tehama Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Geofrey Mpangala mara baada ya kuwasili katika kituo cha Masempele alipokagua uboreshaji wa Daftari la wapiga kura kata ya Ng'ambo mkoani Tabora. Mkurugenzi wa Habari na Elimu ya Mpiga Kura kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bi. Giveness Aswile akipata maelezo kutoka kwa Mohammed Chilongani  BVR Kit Operator katika kituo cha  shule ya sekondari ya Kaze wakati alipotembelea vituo vya uboreshaji wa Daftari la wapiga kura kata ya Ng'ambo mkoani Tabora. ..........................

TANZANIA YAISHUKURU TRADEMARK AFRICA

Image
  Na Benny Mwaipaja, Dar es Salaam Tanzania imeishukuru Taasisi ya Trademark Afrika (TMA) kwa mchango wao katika kuboresha mifumo mbalimbali inayochangia kuimarika kwa mazingira ya biashara uwekezaji nchini. Shukrani hizo zimetolewa jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa inayosimamia utekelezaji wa miradi ya TMA nchini (National Oversight Committee -NOC), Dkt. Natu El-maamry Mwamba, wakati akifungua Mkutano wa Pamoja wa Wenyeviti wa NOC, Bodi ya Wakurugenzi wa TMA na Washirika wa Maendeleo wa TradeMark Afrika (TMA). Dkt. Mwamba alisema kuwa katika kipindi cha mwaka 2022/2023, Serikali imeshuhudia mageuzi makubwa ya kimifumo na kiutendaji kufuatia kukamilika kwa baadhi ya miradi ikiwemo mradi wa kusimika skana ya kupimia mizigo katika mpaka wa Tunduma, mradi wa mfumo wa kutoa vibali vya uwekezaji, na mfumo wa kutoa vibali kwa wafanyabiashara wa mifugo na bidhaa za mifugo, ambayo imeongeza ufanisi wa utoaji huduma. Alisem

MABADILIKO KATIKA TAASISI ZA UMMA YATAONGEZA TIJA: MSAJILI WA HAZINA

Image
  NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, JNICC MSAJILI wa Hazina (TR), Bw. Nehemiah Mchechu amesema, Mabadiliko ya Utendaji (Reforms) yataongeza tija na mafanikio katika utendaji kazi wa Taasisi za Umma. Ameyasema hayo Novemba 28, 2023, kwenye Kikao Kazi na Wahariri wa Vyombo vya Habari nchini katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam. Alisema kimsingi Taasisi ni wazalishaji na zinapaswa kuzalisha kwa ajili kugharamia mipango yao binafsi na ya serikali pia. “Kuna baadhi ya Mashirika yanafanya vizuri, lakini yapo ambayo hayafanyi vizuri, hapa tutaangalia kwanini haya yanafanya vizuri na mengine hayafanyi vizuri, na yale yasiyofanya vizuri itabidi tuchukue hatua.” Alifafanua. Hata hivyo alitoa angalizo kuwa yapo mashirika ya kimkakati ambayo licha ya kutofanya vizuri, serikali haitayaacha itaendelea kuyasimamia na badala yake itafanyia kazi mapungufu yanayosababisha yasifanye vizuri. Alisema muelekeo mpya  wa Ofisi ya Msajili wa Hazina ni k