TANZANIA YAISHUKURU TRADEMARK AFRICA
Na Benny Mwaipaja, Dar es Salaam
Tanzania
imeishukuru Taasisi ya Trademark Afrika (TMA) kwa mchango wao katika kuboresha
mifumo mbalimbali inayochangia kuimarika kwa mazingira ya biashara uwekezaji
nchini.
Shukrani
hizo zimetolewa jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha ambaye pia
ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa inayosimamia utekelezaji wa miradi ya TMA
nchini (National Oversight Committee -NOC), Dkt. Natu El-maamry Mwamba, wakati
akifungua Mkutano wa Pamoja wa Wenyeviti wa NOC, Bodi ya Wakurugenzi wa TMA na
Washirika wa Maendeleo wa TradeMark Afrika (TMA).
Dkt.
Mwamba alisema kuwa katika kipindi cha mwaka 2022/2023, Serikali imeshuhudia
mageuzi makubwa ya kimifumo na kiutendaji kufuatia kukamilika kwa baadhi ya
miradi ikiwemo mradi wa kusimika skana ya kupimia mizigo katika mpaka wa Tunduma,
mradi wa mfumo wa kutoa vibali vya uwekezaji, na mfumo wa kutoa vibali kwa
wafanyabiashara wa mifugo na bidhaa za mifugo, ambayo imeongeza ufanisi wa
utoaji huduma.
Alisema
kuwa kusimikwa kwa mfumo wa skana katika mpaka wa Tunduma, kumepunguza muda wa upimaji
na uondoshaji mizigo kutoka wastani wa siku 5 hadi siku moja huku mradi wa
dirisha moja la kielekroniki la uwekezaji umepunguza muda wa kupata vibali kwa
wawekezaji na kupunguza gharama za kupata
vibali vya uwekezaji nchini.
Dkt.
Mwamba aliyataja mafanikio mengine yanayotokana na uwekezaji wa Trademark
Afrika kuwa ni kuimarika kwa upatikanaji wa masoko ya bidhaa za mbogamboga na
maua kwa kuwaunganisha na masoko ya uhakika wakulima 964 ambao waliuza kilo
milioni 2.1 zenye thamani za zaidi ya shilingi bilioni 3.6.
“Pia
Trademark Africa, wameiwezesha Tanzania kupitia Taasisi ya TMX, kwa kujenga
mfumo wa kimtandao unaowawezesha wakulima kuuza mazao yao ya kilimo na mifugo
kwa faida kupitia mfumo huo na kuwawezesha wakulima kupata faida na Serikali kukusanya
ruzuku” Alisema Dkt. Mwamba
Dkt.
Mwamba alisema kuwa Tanzania imepitia upya na imeboresha mifumo yake ya kodi
hatua iliyochangia kwa kiasi kikubwa kuboresha mazingira ya biashara na kuvutia
uwekezaji na kutoa wito kwa wajumbe wa Mkutano huo, kuimarisha ushirikiano
hususan katika eneo la kukuza biashara na kuboresha mazingira ya uwekezaji ili
kuinua biashara, uchumi na maisha ya wananchi.
Kwa
upande wake, Naibu Afisa Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Program ya Trademark Africa,
Bi. Allen Asiimwe, alisema kuwa katika muongo mmoja uliopita, TMA imewekeza kiasi cha dola za Marekani
bilioni 1.2 ikiwa ni jitihada za kuboresha uzalishaji, kuimarisha biashara na
mazingira ya uwekezaji katika nchi wanachama.
Alisema
kuwa jitihada hizo pamoja na za nchi wanachama bado jitihada kubwa zinahitajika
kwa nchi wanachama kuboresha uuzaji wa bidhaa nje pamoja na kuimarisha mifumo
ya kidigitali inayoweza kuchochea biashara na uwekezaji.
Aliwahakikishia
wajumbe wa mkutano huo kwamba TMA itaendelea kuwekeza katika ujenzi wa miundombinu
kwa nchi wanachama wake ambapo kwa Tanzania, pamoja na miradi mingine, Taasisi
hiyo inatarajia kuwekeza katika ujenzi wa miundombinu ya Bandari ya Dar es
Salaam ili kuongeza zaidi ufanisi wa Bandari hiyo muhimu kwa maendeleo ya nchi
na ukanda mzima wa maziwa makuu.
Bi.
Asiimwe alizungumzia pia umuhimu wa kukuza biashara kwa njia ya mtandao ambayo
imeendelea kukua kwa kasi na kuwavutia vijana wengi zaidi wanaojipatia kipato
kupitia njia hiyo jambo ambalo linaweza kuongeza mapato ya Serikali na kukuza
pia kiwango cha ajira.
Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akizungumza wakati akifungua
Mkutano wa Pamoja wa Wenyeviti wa Bodi ya Wakurugenzi na Washirika wa Maendeleo
wa TradeMark Afrika (TMA), katika Hoteli ya Johari Rotana, jijini Dar es
Salaam, ambapo Wajumbe hao wamejadili kwa pamoja fursa na changamoto za
utekelezaji wa Miradi inayofadhiliwa na TradeMark Afrika, ambayo inalenga
kuwezesha na kuimarisha biashara katika nchi wanachama na namna ya utekelezaji
wa Miradi hiyo pamoja na kuimarisha Miundombinu, Mifumo, Sheria za Biashara na
Uwekezaji, hususan katika kipindi hiki cha utekelezaji wa Soko Huru la Afrika
(AFCFTA).
Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akizungumza wakati akifungua
Mkutano wa Pamoja wa Wenyeviti wa Bodi ya Wakurugenzi na Washirika wa Maendeleo
wa TradeMark Afrika (TMA), katika Hoteli ya Johari Rotana, jijini Dar es
Salaam, ambapo Wajumbe hao wamejadili kwa pamoja fursa na changamoto za
utekelezaji wa Miradi inayofadhiliwa na TradeMark Afrika, ambayo inalenga
kuwezesha na kuimarisha biashara katika nchi wanachama na namna ya utekelezaji
wa Miradi hiyo pamoja na kuimarisha Miundombinu, Mifumo, Sheria za Biashara na
Uwekezaji, hususan katika kipindi hiki cha utekelezaji wa Soko Huru la Afrika
(AFCFTA).
Wajumbe wa Mkutano wa Wenyeviti wa Bodi ya Wakurugenzi na Washirika wa Maendeleo wa TradeMark Afrika (TMA), wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akifungua Mkutano wa Pamoja wa Wenyeviti wa Bodi ya Wakurugenzi na Washirika wa Maendeleo wa TradeMark Afrika (TMA), katika Hoteli ya Johari Rotana, jijini Dar es Salaam, ambapo Wajumbe hao wamejadili kwa pamoja fursa na changamoto za utekelezaji wa Miradi inayofadhiliwa na TradeMark Afrika, ambayo inalenga kuwezesha na kuimarisha biashara katika nchi wanachama na namna ya utekelezaji wa Miradi hiyo pamoja na kuimarisha Miundombinu, Mifumo, Sheria za Biashara na Uwekezaji, hususan katika kipindi hiki cha utekelezaji wa Soko Huru la Afrika (AFCFTA).
Naibu
Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban (Katikati), akifuatilia
kwa makini hotuba ya Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba,
wakati akifungua Mkutano wa Pamoja wa Wenyeviti wa Bodi ya Wakurugenzi na
Washirika wa Maendeleo wa TradeMark Afrika (TMA), katika Hoteli ya Johari
Rotana, jijini Dar es Salaam, ambapo Wajumbe hao wamejadili kwa pamoja fursa na
changamoto za utekelezaji wa Miradi inayofadhiliwa na TradeMark Afrika, ambayo
inalenga kuwezesha na kuimarisha biashara katika nchi wanachama na namna ya
utekelezaji wa Miradi hiyo na kuimarisha Miundombinu, Mifumo, Sheria za
Biashara na Uwekezaji, hususan katika kipindi hiki cha utekelezaji wa Soko Huru
la Afrika (AFCFTA).
Baadhi
ya Wajumbe wa Mkutano wa Wenyeviti wa Bodi ya Wakurugenzi na Washirika wa
Maendeleo wa TradeMark Afrika (TMA), wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Fedha,
Dkt. Natu El-maamry Mwamba, wakati akifungua mkutano wa Pamoja wa Wenyeviti wa
Bodi ya Wakurugenzi na Washirika wa Maendeleo wa TradeMark Afrika (TMA), katika
Hoteli ya Johari Rotana, jijini Dar es Salaam, ambapo Wajumbe hao wamejadili
kwa pamoja fursa na changamoto za utekelezaji wa Miradi inayofadhiliwa na
TradeMark Afrika, ambayo inalenga kuwezesha na kuimarisha biashara katika nchi
wanachama na namna ya utekelezaji wa Miradi hiyo na namna ya kuimarisha
Miundombinu, Mifumo, Sheria za Biashara na Uwekezaji, hususan katika kipindi
hiki cha utekelezaji wa Soko Huru la Afrika (AFCFTA).
Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (Kushoto), akisalimiana
na Naibu Katibu Mkuu, Jumuiya ya Afrika
Mashariki (EAC) anayeshughulikia Masuala ya Forodha, Biashara na Fedha, Bi.
Annette Mutaawe, kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Pamoja wa Wenyeviti wa Bodi ya
Wakurugenzi na Washirika wa Maendeleo wa TradeMark Afrika (TMA), katika Hoteli
ya Johari Rotana, jijini Dar es Salaam.
Comments
Post a Comment