MABADILIKO KATIKA TAASISI ZA UMMA YATAONGEZA TIJA: MSAJILI WA HAZINA

NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, JNICC

MSAJILI wa Hazina (TR), Bw. Nehemiah Mchechu amesema, Mabadiliko ya Utendaji (Reforms) yataongeza tija na mafanikio katika utendaji kazi wa Taasisi za Umma.

Ameyasema hayo Novemba 28, 2023, kwenye Kikao Kazi na Wahariri wa Vyombo vya Habari nchini katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.

Alisema kimsingi Taasisi ni wazalishaji na zinapaswa kuzalisha kwa ajili kugharamia mipango yao binafsi na ya serikali pia.

“Kuna baadhi ya Mashirika yanafanya vizuri, lakini yapo ambayo hayafanyi vizuri, hapa tutaangalia kwanini haya yanafanya vizuri na mengine hayafanyi vizuri, na yale yasiyofanya vizuri itabidi tuchukue hatua.” Alifafanua.

Hata hivyo alitoa angalizo kuwa yapo mashirika ya kimkakati ambayo licha ya kutofanya vizuri, serikali haitayaacha itaendelea kuyasimamia na badala yake itafanyia kazi mapungufu yanayosababisha yasifanye vizuri.

Alisema muelekeo mpya  wa Ofisi ya Msajili wa Hazina ni kubadili Jina na kuwa Mamlaka ya Uwekezaji wa Umma (Public Investments Authority – PIA)

“Katika muundo huu mpya pia tutaanzisha Mfuko wa Uwekezaji wa Umma- (Public Investment Fund ), ambao kazi yake ni kuzisaidia Taasisi kuimarisha mtaji” Alifafanua.

Alisema katika hali ya sasa TR anawajibika kusimamia utendaji wa Taasisi zote za umma,  TR amepewa mamlaka ya kuwekeza katika Taasisi na kusimamia uwekezaji, hata hivyo wigo ni finyu.

“Katika mapendekezo ya muundo mpya, Ofisi ya Msajili wa Hazina sasa itakuwa Mamlaka ya Uwe kezaji wa Umma (Public Investment Authority - PIA) lengo ni kuakisi majukumu na mwenendo wa ukuaji wa uchumi wa duniani.” Alisema.

Alisema ili kuongeza ufanisi katika taasisi hizo mambo manne lazima yazingatiwe ambayo ni kuwa na uongzi bora (Good Leadership), Taasisi kutoingiliwa (kuwa huru), Kuwa na Rasilimali za kutosha (Resources) lakini pia Kupima utendaji (KPI) na kutolea mfano kuhusu kupima utendaji..... tumetengeneza vigezo vipya, zamani kulikuwa na vigezo ambavyo havijazingatia sekta. Unapomsimamia Tanesco au Muhimbili hawa kazi ni tofauti na hadi vigezo vyao. Hivyo ni lazima vigezo viendane na sekta husika na asili ya taasisi inavyofanya kazi yake,” alieleza.

Alirejea kauli yake kuwa mabadiliko katika taasisi za umma hayaepupikiki na kuwataka watendaji kujipanga na kuwa tayari kwa mabadiliko hayo ambayo tayari yameanza.

“Tumeshaanza, mabadiliko mtaona  tunachanganya damu changa na wale wakongwe, na inapobidi tunachukua mtendaji kutoka sekta binafsi kuja kuongoza taasisi ya umma.” Alibainisha. 

Amesema Ofisi yake inashughulika na Watendaji na Wenyeviti wa Bodi, hawa ni watu wazito, hivyo najua kazi itakuwa ngumu lakini lazima mabadiliko yafanyike.

"Mtarajio ya Mhe, Rais ni kuona taasisi hususan zile za kibiashara zinatengeneza faida zitakazozalishwa na kuingizwa Serikalini au kujiendesha pasipo utegemezi wa Serikali kuu, hivyo ni lazima kuwepo mabadiliko ili kuongeza tija na ufanisi" amesema Mchechu.

Kuhsuu majukumu ya Ofisi ya Msajili wa Hazina, alisema Ofisi yake inayo majukumu manne ambayo ni pamoja na Kusimamia, Kumiliki/Kutunza, Kushauri na Kubinafsisha.

Kuna jumla ya Taasisi za Umma 298, ambapo 248 ni Taasisi, Mashirika ya Umma, na Wakala wa Serikali na 50 ni Kampuni ambazo Serikali ina hisa chache, alisema.

“Kampuni zote ambazo Serikali ina umiliki wa hisa chache ni za Kibishara ambapo 40 ziko ndani ya nchi na 10 ziko nje ya nzi.” Alifafanua.

Aidha Taasisi, Mashirika ya Umma, na Wakala wa Serikali 213 ni za utoaji huduma huku 35 ndio za kibishara.

Msaji wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu, akizungumza kwenye Kikao Kazi na Wahariri wa Vyombo vya Habari kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam, Novemba 29, 2023.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Bw. Deodatus Balile, akizungumza kwenye kikao hicho.

Baadhinya watendaji wa Ofisi ya Msajili wa Hazina wakiwa wamejumuika na wahariri

Baadhi ya Wahariri wa Vyombo vya Habari, wakiwa kwenye Kikao Kazi baina ya Wahariri na Msajili wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchecu, kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Novemba 29, 2023.

Baadhi ya Watendaji wa Ofisi ya Msajili wa Hazina, wakiwa pamoja na Wahariri wa Vyombo vya Habari, kwenye Kikao Kazi baina ya Wahariri na Msajili wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchecu, kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Novemba 29, 2023.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Msajili wa Hazina, Bw. Thobias Makoba, akizungumza mwanzoni mwa Kikao Kazi, Baina ya Msajili wa Hazina Bw. Nehemia Mchechu na Wahariri wa vyombo vya Habari kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Novemba 29, 2023.

Mhariri wa gazeti la Jamhuri, Bw. Manyerere Jackton, akizungumza wakati wa kipindi cha maswali na majibu.
Mwenyekiti mstaafu wa TEF, Bw. Absalom Kibanda, akizungumza wakati wa kipindi cha maswali na majibu.

Msaji wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu (kulia) akifurahia jambo na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Bw. Deodatus Balile, kwenye Kikao Kazi na Wahariri wa Vyombo vya Habari kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam, Novemba 29, 2023.

Baadhi ya Watendaji wa Ofisi ya Msajili wa Hazina, wakiwa pamoja na Wahariri wa Vyombo vya Habari, kwenye Kikao Kazi baina ya Wahariri na Msajili wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchecu, kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Novemba 29, 2023.

Comments

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"