Posts

KUTOKA MAGAZETINI OKTOBA 31, 2023

Image
 

WAZIRI MKUU AWAONGOZA VIONGOZI, WABUNGE, WATUMISHI WABUNGE NA WANANCHI MBALIMBALI KATIKA KUMPOKEA RAIS WA IPU JIJINI DODOMA

Image
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, amewaongoza viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali wakiwemo wananchi wa Mkoa wa Dodoma katika mapokezi ya Spika wa bunge Mhe. Dkt. Tulia Ackson, alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma leo Oktoba 30, 2023 akitokea nchuini Anbgola ambapo hivi majuzi alichaguliwa kuwa Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU). Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akisalimiana na kumpongeza Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Dodoma leo Oktoba 30, 2023 akitokea nchini Angola ulikofanyika Mkutano wa 147 wa Umoja huo. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akisalimiana na kumpongeza Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) mara baada ya kuwasili katika uw

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ATEMBELEA BANDA LA CATC

Image
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa amezindua sherehe za miaka 20 Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) na kupata fursa ya kutembelea banda la Maonyesho la Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania(CATC) na kupata  maelezo juu ya Kozi mbalimbali zinazotolewa na chuo hicho kutoka kwa Mkuu wa Mafunzo Chuo cha CATC Bw. Didacus Mweya. Chuo cha CATC kinatoa mafunzo mbalimbali ya muda mfupi katika masuala mbalimbali ya Usafiri wa Anga. Chuo cha CATC ni chuo kinachotambulika kitaifa na Kimataifa chenye ithibati ya  TCAA , NACTVET na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani(ICAO). Na ni miongoni ya vyuo sita Afrika vinavyotambuliwa na ICAO vinavyoa kozi za usalama wa Usafiri wa Anga na miongoni mwa vyuo 35 duniani. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Didacus Mweya Mkuu wa Mafunzo Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC), alipotembelea banda la CATC wakati wa maadhimisho ya miaka 20 y

WADAU KUSHIRIKISHWA MAPITIO YA SERA YA HABARI NA UTANGAZAJI

Image
Na Mwandishi Wetu Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Bw. Mobhare Matinyi amebainisha kuwa, Serikali ipo katika mchakato wa mapitio ya Sera ya Habari na Utangazaji ya mwaka 2003 ambapo imekusudia kushirikisha wadau mbalimbali ikiwemo Mashirika ya Serikali, Vyombo vya Habari, Asasi za Kiraia, Wasomi, Washirika wa Maendeleo na wadau wengine muhimu. Bw. Matinyi ameyasema hayo leo mjini Mororgoro, wakati akizindua kikao kazi cha mapitio ya Sera hiyo kilichoandaliwa na Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kupitia Idara ya Habari (MAELEZO) kwa kushirikiana na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO). Aidha amebainisha kuwa, katika mchakato huo, hatua mbalimbali zitafanyika ikiwemo uchambuzi wa kina wa sera iliyopo, utafiti wa kitaaluma, na kuzingatia viwango bora vya kimataifa katika vyombo vya habari na utangazaji. “Vilevile mafunzo na mashauriano ya wadau yatafanyika kwa maafisa wanaohusika na mapitio ya Sera pamo

MAONESHO YA SANAA ZIWANI NYANZA YAFANYIKA MWANZA

Image
  Maonesho ya Sanaa Ziwani Nyanza yaliyohusisha michoro mbalimbali pamoja na uzinduzi wa sanamu ya mvuvi akiwa kwenye mtumbwi yamefanyika jijini Mwanza kwa lengo la kuelimisha jamii kutunza mazingira likiwemo Ziwa Victoria. Maonesho hayo yamefanyika Jumamosi Oktoba 28, 2023 katika ufukwe wa Kamanga yakiandaliwa na shirika la mazingira na maendeleo EMEDO lililotoa mafunzo kwa wasanii wa michoro jijini Mwanza kwa kushirikiana na taasisi ya NAAM Festiva ya Kenya na Wasanii Visual Arts ya Dar es salaam   kupitia mradi wa Sanaa Ziwani Nyanza unaofadhiliwa na ubalozi za Uswis na Noray nchini Tanzania. Afisa mradi wa Sanaa Ziwani Nyanza kutoka shirika la EMDEO, Urthur Mjema amesema lengo la mradi huo ni kutumia sanaa ya michoro kuhamasisha jamii kuhusu utunzaji wa mazingira na hasa Ziwa Victoria kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo. "Tusipotunza Ziwa hili halitakuwa na manufaa miaka ijayo kutokana na athari zinazoweza kusababisha vifo kwa viumbe hai ikiwemo samaki na dagaa. Tuna waj