WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ATEMBELEA BANDA LA CATC

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa amezindua sherehe za miaka 20 Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) na kupata fursa ya kutembelea banda la Maonyesho la Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania(CATC) na kupata  maelezo juu ya Kozi mbalimbali zinazotolewa na chuo hicho kutoka kwa Mkuu wa Mafunzo Chuo cha CATC Bw. Didacus Mweya.

Chuo cha CATC kinatoa mafunzo mbalimbali ya muda mfupi katika masuala mbalimbali ya Usafiri wa Anga. Chuo cha CATC ni chuo kinachotambulika kitaifa na Kimataifa chenye ithibati ya  TCAA , NACTVET na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani(ICAO). Na ni miongoni ya vyuo sita Afrika vinavyotambuliwa na ICAO vinavyoa kozi za usalama wa Usafiri wa Anga na miongoni mwa vyuo 35 duniani.


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Didacus Mweya Mkuu wa Mafunzo Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC), alipotembelea banda la CATC wakati wa maadhimisho ya miaka 20 ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania. Kushoto kwake ni Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa Mnyaa.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akipokea zawadi kutoka Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) aliyowasilishwa na Mkuu wa kitengo cha leseni za Usafiri wa Anga Mossy Kitang’ita alipotembelea banda la CATC wakati wa maadhimisho ya miaka 20 ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania.

Comments

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"