WCF YATWAA TUZO SIKU YA KIMATAIFA YA USALAMA NA AFYA MAHALI PA KAZI
NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, MOROGORO MFUKO wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) umetwaa tuzo ya Mfuko Bora miongoni mwa Taasisi za Bima na Fidia wakati wa kilele cha Siku ya Kimataifa ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi kwenye viwanja vya Tumbaku mjini Morogoro ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Profesa Joyce Ndalichako. Kilele cha Maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Usalama na Afya mahali pa kazi hufanyika Aprili 28 kila mwaka ambapo Tanzania huungana na mataifa mengine duniani kuiadhimisha siku hii, lengo kubwa ni kuendeleza kampeni za kuhamasisha uwepo wa mazingira salama na yenye kulinda afya za watu katika sehemu za kazi ambapo kauli mbiu ya maadhimisho kwa mwakam huu ni “Mazingira salama na afya ni kanuni na haki ya msingi mahali pa kazi.”. Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma alipokea tuzo hiyo kutoka kwa mgeni rasmi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira, na Wenye Ulemavu), Profesa Joyc