WCF YATWAA TUZO SIKU YA KIMATAIFA YA USALAMA NA AFYA MAHALI PA KAZI
NA
K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, MOROGORO
MFUKO wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) umetwaa tuzo ya Mfuko Bora miongoni mwa Taasisi za Bima na Fidia wakati wa kilele cha Siku ya Kimataifa ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi kwenye viwanja vya Tumbaku mjini Morogoro ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Profesa Joyce Ndalichako.
Kilele
cha Maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Usalama na Afya mahali pa kazi
hufanyika Aprili 28 kila mwaka ambapo Tanzania huungana na mataifa mengine
duniani kuiadhimisha siku hii, lengo kubwa ni kuendeleza kampeni za kuhamasisha
uwepo wa mazingira salama na yenye kulinda afya za watu katika sehemu za kazi
ambapo kauli mbiu ya maadhimisho kwa mwakam huu ni “Mazingira salama na afya ni
kanuni na haki ya msingi mahali pa kazi.”.
Mkurugenzi
Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma alipokea tuzo hiyo kutoka kwa mgeni rasmi, Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira, na Wenye Ulemavu), Profesa
Joyce Ndalichako.
Akizungumza
baada ya kutwaa tuzo hiyo, Mkurugenzi wa Huduma za Tiba WCF, Dkt. Abdulsalaam
Omar alisema Tuzo hiyo ni faraja kwa Wafanyakazi na Mfuko kwa ujumla imeonyesha
jinsi mifumo ya kudhibiti ajali na magonjwa mahali pa kazi ni madhubuti.
“Hii
inatupa matumaini na inatupa moyo zaidi kuendelea kuboresha maeneo ya kazi na
kwakuwa WCF ni mdau mkubwa katika masuala haya hatuishii hapa tu kwa wafanyakazi
wetu bali kwa wafanyakazi wengine ambao ni wadau wakubwa wa Mfuko.” Alifafanua.
Comments
Post a Comment