Posts

RAIS SAMIA AFANYA MAZUNGUMZO NA MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE. KAMALA HARRIS, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Image
  Makamu wa Rais wa Marekani, Mhe. Kamala Harris ameeleza kuwa Rais wa Marekani, Joe Biden anajivunia uongozi imara unaodumisha amani na demokrasia nchini Tanzania chini ya Rais wa sasa, Dkt. Samia Suluhu Hassan. Akizungumza Ikulu jijini Dar es Salaam, Tanzania alipokutana na mwenyeji wake Rais Samia, Makamu wa Rais, Kamala amasema kuwa taifa la Marekani linajivunia uhusiano mzuri uliopo kati yao na Tanzania, uhusiano uliodumishwa tangu enzi za aliyekuwa Rais wa 35 wa Marekani miaka ya 1961-1963. “Marekani inajivunia uhusiano imara uliopo kati yake na Tanzania, uhusiano uliotukuka kati yetu unatokana na uongozi bora na demokrasia imara iliyopo baina yetu. Marekani tunakupongeza Mhe. Samia kuwa Kiongozi bora katika taifa hili la Tanzania,” amesema Makamu wa Rais wa Marekani, Mhe. Kamala  “Tanzania mmekuwa kipaumbele kwenye utawala bora na suluhisho na mageuzi kwenye suala la demokrasia, na ndio maana Rais Joe Biden anajivunia wewe Kiongozi, Mhe. Samia Suluhu Hassan,” ameeleza Mhe. Kamal

SAMIA NA HARRIS WADHAMIRIA KUIMARISHA USHIRIKIANO

Image
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa rai kwa Serikali ya Marekani kufanya marejeo ya mkataba wa Mpango wa Ukuzaji Fursa za Kiuchumi Afrika (African Growth and Opportunity Act - AGOA) na kuuhuisha hadi mwaka 2030. Rais Samia ametoa rai hiyo leo wakati akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kumpokea mgeni wake Mhe. Kamala Harris, Makamu wa Rais wa Marekani ambae yuko katika ziara ya kikazi nchini. Aidha, Rais Samia amesema mpango wa AGOAambao unaisha mwaka 2025 ni muhimu kwa Tanzania kwa kuwa ni njia pekee ya biashara ambayo bara la Afrika linautegemea kujikomboa kutoka lindi la umaskini. Vile vile, Rais Samia ametoa wito kwa Marekani kufanya mapitio ya Mkataba wa Viza ili kuwawezesha raia wa mataifa yote mawili kunufaika na viza ya muda mrefu kwakuongeza ukuaji wa biashara, utalii na uwekezaji. Rais Samia pia ameishukuru Marekani kwa msaada wanaoutoa katika kuleta maendeleo nchini kwenye sekta za afya, elimu, maji, usafi wa mazingira, kilimo

KAMATI YA PIC YARIDHISHWA NA MRADI WA KITEGAUCHUMI CHA JENGO LA KIBIASHARA (THE ROCK CITY MALL) LA PSSSF

Image
NA MWINDISHI WETU, MWANZA KAMATI ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (Public Investment Committee PIC) imepongeza uwekezaji uliofanywa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kwenye Mradi wa kitegauchumi cha jengo la kibiashara (the rock city mall) jijini mwanza. Wajumbe hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa PIC, Mhe. Jerry Silaa wametoa pongezi hizo Machi 30, 2023 baada kutembelea mradi huo kwa lengo la kuona tija iliyopo kwenye uwekezaji huo.  Walisema uwekezaji wa jengo hilo umebadilisha sura ya jiji la Mwanza  ambapo zamani eneo hilo lilitapakaa vibanda tu na kwamba uwekezaji umebadilisha sura ya jiji la Mwanza jambo ambalo limeleta thamani ya kijamii (social value),” alisema Aidha wamesema uwekezaji wa mradi wa “the rock city mall” ni moja ya miradi iliyokamilika na yenye kutia matumaini hata hivyo walishauri kufanywe marekebisho sehemu ambazo zina mapungufu ili kuvutia wapangaji kwenye maeneo ambayo bado hayana wapangaji. Walioungana na Menejimenti juu ya athari

WAZIRI TABIA MAULID MWITA AWATAKA MAAFISA HABARI SERIKALINI KUHUWISHA TAARIFA KWENYE TOVUTI NA MITANDAO YA KIJAMII YA SERIKALI

Image
NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID WAZIRI wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Tabia Maulid Mwita amefunga Kikao Kazi cha 18 cha Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano kutoka Serikalini (TAGCO) na kuwataka kuhuwisha taarifa zilizomo kwenye tovuti na mitandao ya kijamii ya Serikali. Ameyasema hayo Machi 30, 2023 mbele ya washiriki kutoka Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Darves Salaam . “Niwangapi kati yenu ambao mmetekeleza agizo la Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye aliyewataka kuhakikisha taarifa za serikali zinawekwa mara kwa mara kwenye tovuti na mitandao ya kijamii ili kuwa na ufanisi katika kutumia njia za kisasa za mawasilino katika utoaji taarifa kwa umma?.” Aliuliza. Alisema anaungana na Mhe. Nape ambaye alisema baadhi ya tovuti na mitandao hiyo ya serikali ina taarifa za muda mrefu zilizopitwa na wakati. “Tuna kazi kubwa mbele yet

MBUNGE MASANJA AGAWA MITUNGI 100 YA GESI KWA WAJASIRIAMALI NA VIFAA VYA MICHEZO KWA SHULE TATU WILAYANI UKEREWE

Image
 NA MWANDISHI WETU, MWANZA Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mwanza na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Mary Masanja amegawa mitungi ya gesi 100 kwa wanawake wajasiriamali na Vifaa vya Michezo kwa shule tatu Wilayani Ukerewe jana Machi 29, 2023 ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake za kuwawezesha wajasiriamali na kuunga mkono masuala ya michezo mashuleni Mkoani Mwanza. Vifaa hivyo vya michezo vilivyokabidhiwa kwa shule za Sekondari za Nansio, Bukongo na Namagondo ni pamoja na mipira na jezi vyenye thamani ya shilingi milioni 3,350,000. Pia katika ziara hiyo, Mhe. Masanja amekabidhi fedha taslimu kiasi cha shilingi milioni 3,000,000 kwa ajili ya kuwasaidia wajasiriamali hao kuendelea kujinunulia nishati gesi kwa ajili ya biashara zao. Awali akizungumza na wanafunzi hao, Mhe. Masanja aliwaasa kusoma kwa bidii,kuwa na hofu ya Mungu , nidhamu na kuwaonya kutojihusisha na mambo ambayo sio utamaduni wa Mtanzania. Aidha aliwataka wajasiriamali kutumia nishati mbadala na kuachana na matum

MTANDAO WA MASHIRIKA YA KAIRUKI (KHEN) WAJIPAMBANUA KIMATAIFA

Image
  Balozi wa Tanzania nchini Sudan kusini Balozi John Simbachawene kushoto akimpongeza Bw. Benson Meikoki Meneja Mauzo na Masoko Kiwanda cha madawa cha Kairuki (KPIL) mara baada ya kuwasilisha mada Katika kongamano la msafara wa kibiashara wa Tanzania uliotembelea nchini Sudan Kusini Katika jiji la Juba ili kuangalia fursa mbalimbali za kibiashara na uwekezaji Katika sekta ya Kilimo afya na Elimu. Bw. Benson Meikoki Meneja Mauzo na Masoko Kiwanda cha madawa cha Kairuki (KPIL) kilichopo chini ya mtandao wa mashirika ya Kairuki (KHEN) akiwasilisha mada Katika kongamano la msafara wa kibiashara wa Tanzania uliotembelea nchini Sudan Kusini Katika jiji la Juba ili kuangalia fursa mbalimbali za kibiashara na uwekezaji Katika sekta ya Kilimo afya na Elimu. Balozi wa Tanzania nchini Sudan kusini Balozi John Simbachawene akiwa Katika picha ya pamoja na Bw. Benson Meikoki Meneja Mauzo na Masoko Kiwanda cha madawa cha Kairuki (KPIL) mara baada ya kuwasilisha mada Katika kongamano la msafara wa

KUTOKA MAGAZETINI LEO ALHAMISI MACHI 30, 2023

Image