RAIS SAMIA AFANYA MAZUNGUMZO NA MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE. KAMALA HARRIS, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

 Makamu wa Rais wa Marekani, Mhe. Kamala Harris ameeleza kuwa Rais wa Marekani, Joe Biden anajivunia uongozi imara unaodumisha amani na demokrasia nchini Tanzania chini ya Rais wa sasa, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza Ikulu jijini Dar es Salaam, Tanzania alipokutana na mwenyeji wake Rais Samia, Makamu wa Rais, Kamala amasema kuwa taifa la Marekani linajivunia uhusiano mzuri uliopo kati yao na Tanzania, uhusiano uliodumishwa tangu enzi za aliyekuwa Rais wa 35 wa Marekani miaka ya 1961-1963.

“Marekani inajivunia uhusiano imara uliopo kati yake na Tanzania, uhusiano uliotukuka kati yetu unatokana na uongozi bora na demokrasia imara iliyopo baina yetu. Marekani tunakupongeza Mhe. Samia kuwa Kiongozi bora katika taifa hili la Tanzania,” amesema Makamu wa Rais wa Marekani, Mhe. Kamala 

“Tanzania mmekuwa kipaumbele kwenye utawala bora na suluhisho na mageuzi kwenye suala la demokrasia, na ndio maana Rais Joe Biden anajivunia wewe Kiongozi, Mhe. Samia Suluhu Hassan,” ameeleza Mhe. Kamala

Aidha, Mhe. Kamala amesema uhusiano huo uliopo ni hamasa na hamu ya kuchochea ukuaji wa masuala ya Uchumi nchini Tanzania sanjari na kukaa na kujadili kwa kina changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi ambayo mara kadhaa imekuwa na athari kubwa ulimwenguni.

Makamu wa Rais wa Marekani, Mhe. Kamala Harris yupo nchini Tanzania tangu, Machi 29, 2023, ataondoka nchini Machi 31, 2023 baada ya kumaliza ziara yake nchini hapa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mgeni wake Makamu wa Rais wa Marekani Mhe. Kamala Harris mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa Kikwete Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 30 Machi, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mgeni wake Makamu wa Rais wa Marekani Mhe. Kamala Harris mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa Kikwete Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 30 Machi, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mgeni wake Makamu wa Rais wa Marekani Mhe. Kamala Harris mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 30 Machi, 2023.





Comments

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"