Posts

TCRA Yashiriki Mbio Za Mwenge Maalum 2021 Ipagala Jijini Dodoma

Image
  Afisa Mwandamizi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)Mabel Masasi  akikabidhi kitabu cha Mwongozo wa Huduma kwa Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Tanzania kwa viongozi wa Mbio za Mwenge Maalum 2020/21 ikiwa ni ishara ya TCRA kuunga mkono kauli mbiu ya mbio za mwenge mwaka huu isemayo "TEHAMA ni msingi wa Taifa endelevu; itumike kwa usahihi na uwajibikaji" Afisa Mawasiliano Mwandamizi  wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mabel Masasi akiwapa maelezo viongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru ulipowasili katika  Shule ya Msingi Ipangala 'B' iliyopo jijini Dodoma wakati wa mbio za Mwenge Maalum 2020/21 ikiwa ni ishara ya TCRA kuunga mkono kauli mbiu ya mbio hizo isemayo "TEHAMA ni msingi wa wa Taifa endelevu; itumike kwa usahihi na uwajibikaji" Baadhi ya viongozi wakipata huduma za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Wakati Mwenge wa Uhuru ulipokwenda katika Shule ya Msingi ya Ipagala B jijini Dodoma. Baadhi ya viongozi wakipata huduma za Mamlaka ya M

KUTOKA MAGAZETINI LEO ALHAMISI JULAI 29, 2021

Image
 

RAIS SAMIA AZINDUA MIRADI ILIYOFADHILIWA NA UJERUMANI KWA JWTZ

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa MAJESHI ya Ulinzi, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikata Utepe kwa ajili ya kupokea Miradi iliyofadhiliwa na kujengwa na Serikali ya Ujerumani kupitia Jeshi la Nchi hiyo (GAFTAG) kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ Lugalo Jijini Dar es salaam leo Julai 28,2021. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa MAJESHI ya Ulinzi, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiondoa kitambaa kwa ajili ya kupokea Miradi iliyofadhiliwa na kujengwa na Serikali ya Ujerumani kupitia Jeshi la Nchi hiyo (GAFTAG) kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ Lugalo Jijini Dar es salaam leo Julai 28,2021. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa MAJESHI ya ulinzi, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipata maelezo  kuhusu uchunguzi wa Magonjwa Ambukizi baada ya kupokea Miradi iliyofadhiliwa na kujengwa na Serikali ya Ujerumani kupitia Jeshi la Nchi hiyo (GAFTAG) kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ Lugalo Jijini Dar es salaam leo Ju

CHANJO DHIDI YA COVID 19: RAIS SAMIA AONYESHA NJIA, APEWA CHANJO HADHARANI

Image
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, leo Julai 28, 2021, amechanja Chanjo dhidi ya Uviko 19, katika hafla ya uzinduzi wa Chanjo hiyo hapa nchini iliyofanyika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam. Viongozi wengine waliochanja ni pamoja na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa na mkewe mama Mary, Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Mizengo Pinda na mkewe mama Tunu, Waziri wa Afya, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima, Waziri wa Mambo ya Nje, Mhe. Liberata Mulamula, Jaji Mkuu, Mhe. Profesa Ibrahim Juma, Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Amos Makala na wakuu wote wa wilaya wa Mkoa wa Dar es Salaam, viongozi wa dini   akiwemo Sheikh Mkuu Mufti Aboubakar Bin Zubeir na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Kanisa Katoliki, Yuda Thadeus Rwaichi na waandishi wa habari. “Leo tunazindua uchanjaji Tanzania tukijua chanjo ni ndogo ukilinganisha na idadi ya Watu, kama alivyosema Waziri, wapo wanaozikataa lakini wanaozitaka ni wengi sana, nina mesej

MHANDISI MASAUNI AAGIZA MIKOPO NA MADENI YA BENKI YA TIB KUREJESHWA

Image
  Na Peter Haule, WFM, Dar es Salaam Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhandisi Hamad Yussuf Masauni, ameiagiza Benki ya TIB kuhakikisha madeni na fedha zote za mikopo zaidi ya shilingi bilioni 535.3 zilizokopeshwa kwa wateja wao bila kufuata taratibu pamoja na wadaiwa sugu zinarejeshwa ili zitumike kutoa mikopo kwenye maeneo mengine yenye tija. Mhandisi Masauni ametoa maagizo hayo jijini Dar es Salaam  alipotembelea  Benki ya TIB  ambapo alikutana na kufanya mazungumzo na Menejimenti ya Benki hiyo na wafanyakazi, katika mwendelezo wa ziara zake za kutembelea taasisi zilizo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango, jijini Dar es Salaam. “Kwa njia yeyote ile ni lazima fedha za wananchi zirejeshwe hivyo nawaagiza pia kuleta mapendekezo Serikalini ili kuangalia iwapo kuna eneo ambalo Serikali inaweza kuingilia kati kuhakikisha tunaokoa fedha za wananchi zilizowekezwa katika miradi isiyo na tija”, alieleza Mhandisi Masauni. Alisema kuwa nchi inapoelekea inahitaji kuona Benki ya TIB inashiriki ki

Benki ya Equity (T) yazindua huduma mpya za kutuma Fedha Kimataifa.

Image
• Kupitia Huduma za “Equity ni Moja” Wateja Benki ya Equity Tanzania  sasa wanaweza kufanya miamala yao katika matawi yote ya Benki ya Equity Congo DRC, Kenya, Uganda, Rwanda, Sudani ya Kusini kama wapo nyumbani. • Kupitia huduma mpya ya SADCC- SIRESS wateja wa Benki ya Equity wanaweza  kufanya miamala kwenda na kutoka katika nchi  SADC kwa gharama ya DOLA 10 tu bila kujali kiwango. Dar es Salaam, Jumanne tarehe 27 Julai 2021 . Benki ya Equity Tanzania leo imeingiza sokoni la huduma mbili mpya za utumaji fedha kimataifa  zinazolenga kuingusha Tanzania na nchi nyingine za Afrika. Huduma hizo ni “Equity ni Moja” ” ambayo inawawezesha Wateja Benki ya Equity Tanzania  kufanya miamala yao katika matawi yote ya Benki ya Equity Congo DRC, Kenya, Uganda. Pia Huduma ya SADCC-SIRESS INAYOWAWEZESHA wateja wa Benki ya kufanya miamala kwenda na kutoka katika nchi  SADC kwa gharama ya DOLA 10 tu bila kujali kiwango. Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Equity (T) Robert Kiboti alisema: "Tunajivunia

RC RUKWA, JOSEPH MKIRIKITI AAGIZA MIRADI INAYOTEKELEZWA MKOANI HUMO ILINGANE NA THAMANI YA FEDHA

Image
HALMASHAURI za mkoa wa Rukwa zimetakiwa kutumia fedha za serikali kuu na za makusanyo ya ndani kukamilisha miradi ya maendeleo kwa kuzingatia thamani ya fedha huku miradi hiyo ikiwemo ujenzi wa shule, ujenzi wa hospitali na miradi ya maji ikiwa na ubora . Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joseph Mkirikiti   (27.07.2021) wakati alipofanya ziara ya kikazi kukagua miradi ya maendeleo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga ikiwa na lengo la kufuatilia na kutilia mkazo utekelezaji wa kazi za Serikali tangu alipoteuliwa kuongoza mkoa wa Rukwa hivi karibuni. Mkuu huyo wa Mkoa ameziagiza Halmashauri mkoani Rukwa kutumia fedha zake za makusanyo ya ndani kuhakikisha miradi ya maendeleo inakamilishwa kwa ubora na wakati ili kero za wananchi kukosa madarasa, maji na huduma za afya ikiwemo ukosefu wa madawa. “Sasa Serikali imepunguza mzigo kwa halmashauri kwa kulipa posho za madiwani hivyo tunategemea kuona fedha iliyokuwa ikilipwa kwao ikitumika kukamilisha miradi ya maendel

AWLN, TAASISI YA MWALIMU NYERERE ZAPEWA CHANGAMOTO YA KUSIMAMIA AMANI AFRIKA

Image
Na Mwandishi wetu, Dar Mtandao wa Uongozi wa Wanawake Afrika (AWLN) kwa kushirikiana na Taasisi ya Mwalimu Nyerere umepewa changamoto ya kukuza na kusimamia masuala ya umoja na amani katika Bara la Afrika ili kuleta maendeleo ya watu.   Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula ametoa wito huo wakati alipokutana na Mtandao huo pamoja na Taasisi ya Mwalimu Nyerere ikishirikiana na Shirika la Kimataifa la kutetea Haki na Maendeleo ya Wanawake (UN Women) leo jijini Dar es Salaam “Agenda yetu ni muhimu, hamuwezi kusema kuwa tuna maendeleo kama hakuna amani…….amani ni sehemu ya Diplomasia ya Uchumi, kama amani huwezi kuitafuta kwa njia nyingine tuseme amani ni maendeleo na maendeleo ni amani,” Amesema Balozi Mulamula Balozi Mulamula ameongeza kuwa, kwa kuzingatia kwamba amani ni matokeo ya haki juhudi zinahitajika katika kuhamasisha na kuunga mkono ushiriki kamili wa wanawake kama wadau muhimu wa kulinda na kutetea amani. Kwa upande wake, Mkurugenzi

MABULA ASIKILIZA KILIO CHA WANA MASASI NA KUTOA MAAGIZO

Image
  Na   Munir Shemweta, MASASI Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amesikiliza kilio cha wananchi wa wilaya ya Masasi kuhusiana na migogoro ya ardhi na na kumuagiza Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Mtwara Rehema Mwinuka kufuatilia utendaji kazi wa sekta ya ardhi katika halmashauri za mkoa wa Mtwara. Akizungumza katika mkutano wa hadhara wakati wa kusikiliza na kuzipatia ufumbuzi changamoto za sekta ya ardhi katika wilaya ya Masasi Julai 27, 2921 mkoani Mtwara, Dkt Mabula alisema  katika ziara yake wilayani humo amebaini uonevu unaofanywa na baadhi ya watumishi wa sekta ya ardhi wasio waaminifu kutowatendea haki wananchi wakati wa kushughulikia changamoto za ardhi. ‘’Hapa nimegundua kuna jambo moja na nakuelekeza Kamishna wa Ardhi fuatilia katika halmashauri zako zote kuna uonevu mkubwa kwenye maeneo ya wananchi, kwa sababu hoja zote zinazoongelewa hapa ni shamba langu limechukuliwa sikupewa chochote au shamba langu ekari sita nimepewa kiwanja kimoja