CHANJO DHIDI YA COVID 19: RAIS SAMIA AONYESHA NJIA, APEWA CHANJO HADHARANI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, leo Julai 28, 2021, amechanja Chanjo dhidi ya Uviko 19, katika hafla ya uzinduzi wa Chanjo hiyo hapa nchini iliyofanyika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Viongozi wengine waliochanja ni pamoja na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa na mkewe mama Mary, Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Mizengo Pinda na mkewe mama Tunu, Waziri wa Afya, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima, Waziri wa Mambo ya Nje, Mhe. Liberata Mulamula, Jaji Mkuu, Mhe. Profesa Ibrahim Juma, Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Amos Makala na wakuu wote wa wilaya wa Mkoa wa Dar es Salaam, viongozi wa dini 
 akiwemo Sheikh Mkuu Mufti Aboubakar Bin Zubeir na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Kanisa Katoliki, Yuda Thadeus Rwaichi na waandishi wa habari.

“Leo tunazindua uchanjaji Tanzania tukijua chanjo ni ndogo ukilinganisha na idadi ya Watu, kama alivyosema Waziri, wapo wanaozikataa lakini wanaozitaka ni wengi sana, nina meseji nyingi watu wakiuliza Mama chanjo lini chanjo lini.... lini, alisema Mhe. Rais Samia katika hotuba yake ya uzinduzi. 

“Niwahakikishie Watanzania wale wote ambao kwa hiari yao wapo tayari kuchanjwa tutahakikisha chanjo zinapatikana, chanjo ni hiari ya mtu lakini pia chanjo ni imani, mwilini mwangu hii chanjo ya leo ni ya sita, tulichanjwa tangu nikiwa Shule ya Msingi na zimenipa uzima wa kutosha kwa miaka 61 mpaka leo nipo hapa." Alisema Rais Samia
na kuongeza...Mimi ni mama wa watoto wanne wanaonitegemea ni bibi wa wajukuu kadhaa, wanaonipenda sana na ninawapenda sana, ni mke pia na ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznia na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya nchi hii nisingejitoa na kujipeleka kwenye hatari kwenye kifo nikijua kwamba nina majukumu yote haya, kama mama, kama bibi, kama mke na kama RAIS na amiri jeshi Mkuu, lakini nimetoka kuonyesha Umma." Alisisitiza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akionesha Cheti cha Uthibitisho wa Chanjo muda mfupi baada ya kuzindua Chanjo ya Uviko 19 katika Viwanja vya Ikulu Jijini Dar es salaam leo Julai 28,2021
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akipata Chanjo ya Uviko 19 katika Viwanja vya Ikulu Jijini Dar es salaam leo Julai 28,2021. Picha na Ikulu.

Comments

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"