RC RUKWA, JOSEPH MKIRIKITI AAGIZA MIRADI INAYOTEKELEZWA MKOANI HUMO ILINGANE NA THAMANI YA FEDHA
HALMASHAURI za mkoa wa Rukwa zimetakiwa kutumia fedha za serikali kuu na za makusanyo ya ndani kukamilisha miradi ya maendeleo kwa kuzingatia thamani ya fedha huku miradi hiyo ikiwemo ujenzi wa shule, ujenzi wa hospitali na miradi ya maji ikiwa na ubora . Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joseph Mkirikiti (27.07.2021) wakati alipofanya ziara ya kikazi kukagua miradi ya maendeleo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga ikiwa na lengo la kufuatilia na kutilia mkazo utekelezaji wa kazi za Serikali tangu alipoteuliwa kuongoza mkoa wa Rukwa hivi karibuni. Mkuu huyo wa Mkoa ameziagiza Halmashauri mkoani Rukwa kutumia fedha zake za makusanyo ya ndani kuhakikisha miradi ya maendeleo inakamilishwa kwa ubora na wakati ili kero za wananchi kukosa madarasa, maji na huduma za afya ikiwemo ukosefu wa madawa. “Sasa Serikali imepunguza mzigo kwa halmashauri kwa kulipa posho za madiwani hivyo tunategemea kuona fedha iliyokuwa ikilipwa kwao ikitumika kukamilisha miradi ya maendel