DORIA YA KUFUKUZA TEMBO KUANZA LEO WILAYANI NACHINGWEA


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akimsikiliza Mhifadhi wa Makumbusho ya Majimaji na ya Kumbukumbu ya Dkt. Rashid Mfaume Kawawa, Balthazar Nyamusya (kushoto) akitoa maelezo kuhusu zana za mishale zilizotumika kipindi cha vita ya Majimaji, alipofanya ziara ya kikazi ya kukagua eneo la Makumbusho ya Majimaji lililopo Bombambili Wilaya ya Songea.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akimsikiliza Mhifadhi wa Makumbusho ya Majimaji na ya Kumbukumbu ya Dkt. Rashid Mfaume Kawawa, Balthazar Nyamusya (kushoto) akitoa maelezo kuhusu handaki lililopo kwenye Makumbusho ya Dkt. Rashid Mfaume Kawawa alipofanya ziara ya kikazi ya kukagua eneo hilo lililopo Bombambili Wilaya ya Songea .

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akimsikiliza Mhifadhi wa Makumbusho ya Majimaji na ya Kumbukumbu ya Dkt. Rashid Mfaume Kawawa, Balthazar Nyamusya (kulia) akitoa maelezo kuhusu mavazi yaliyopo kwenye Makumbusho ya Dkt. Rashid Mfaume Kawawa, wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua Makumbusho hiyo iliyopo eneo la Bombambili Wilaya ya Songea.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akiangalia mnara wa kumbukumbu waliponyongwa mashujaa wa Vita vya Majimaji alipofanya ziara ya kikazi ya kukagua eneo hilo lililopo Wilaya ya Songea. Kulia ni Mhifadhi wa Makumbusho ya Majimaji na Makumbusho ya Kumbukumbu ya Dkt. Rashid Mfaume Kawawa, Balthazar Nyamusya.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akiongoza msafara kupanda Mlima Matogoro katika Hifadhi ya Misitu ya Milima ya Matogoro iliyopo kwenye Manispaa ya Songea. Nyuma yake ni Kamishna Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Prof. Dos Santos Silayo.

************************************

Doria ya Askari wa Wanyamapori kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) inatarajiwa kuanza leo ili kufukuza tembo waliovamia kijiji cha Mbute na Ngulichile Wilayani Nachingwea .

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) wakati wa ziara ya kikazi ya kusikiliza changamoto za wananchi iliyofanyika leo Wilayani Nachingwea.

“Ninawaagiza askari wa wanyamapori kuhakikisha mnaweka kambi katika vijiji hivi na kuanzia leo mfanye doria ya kuangalia tembo walipo ili kuwarudisha katika maeneo yao ya hifadhi” Mhe. Masanja amefafanua.

Amesema doria hizo zitakuwa mwarobaini wa kutatua tatizo la tembo waliovamia makazi ya wananchi katika vijiji hivyo.

“Kambi hii a askari wa wanyamapori katika maeneo haya iwe ya kudumu lakini naelekeza askari waje leo kufukuza tembo ili wananchi waishi kwa amani” amesisitiza mhe. Mary Masanja.

Mhe. Masanja amemuomba Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea pamoja na wananchi wa Wilaya hiyo kutoa ushirikiano wa kutosha ili kukamilisha zoezi hilo.

Aidha, Mhe. Mary Masanja amewaagiza wananchi hao kuanza utamaduni wa kufuga nyuki ili kukabiliana tembo.

“Nawaagiza watakapokuja wakufunzi kutoka Wizarani kuwafundisha mbinu mbalimbali za kukabiliana na tembo, mkubali njia hii ya kufuga nyuki kwa sababu nyuki ni adui wa tembo, sehemu ambayo nyuki yupo tembo hawezi kukaa” Mhe. Mary Masanja ameongeza.

Amefafanua kuwa ufugaji nyuki utasaidia kurutubisha mazao yao korosho wanayolima ili yaweze kukua vizuri.

Akizungumzia kuhusu changamoto ya tembo, Diwani wa Kata ya Ngulichile, Mhe. Said Mwakayola amesema kuwa wananchi wanaogopa kwenda kwenye maeneo yao ya shughuli za kila siku kama kisimani na mashambani kutokana na tatizo hilo la tembo.

“Zoezi hili la kufukuza tembo naomba lianze haraka iwezekanavyo kwa sababu watu wanashindwa kwenda hata kwenye mashamba ya mikorosho kuangalia mazao yao kwa sababu ya tembo hawa” amefafanua Mhe. Mwakayola.

Pia, Mhe. Mwakayola ameahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa askari wa wanamapori watakaoanza zoezi hilo la kukabiliana na tembo.

Ziara hiyo ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja ni mwendelezo wa ziara zake za kikazi za kutatua changamoto ya wanyamapori wakali na waharibifu kama tembo wanaovamia makazi ya wananchi katika sehemu mbalimbali nchini.

Comments

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"