7/28/2021

WAZIRI MKENDA AIELEKEZA TUME YA TAIFA YA UMWAGILIAJI KUWEKA MIUNDOMBINU KWENYE SHAMBA LA PILIPILI MOROGORO

 

Waziri wa Kilimo Mhe. Prof Adolf Mkenda akikagua eneo la kilimo cha Pilipili ambalo lipo chini ya Umoja wa Wajasiriamali wahitimu wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUGECO) kwa ajili ya kilimo cha Pilipili katika kijiji cha Luhindo kilichopo katika Wilaya ya Mvomero, Wakati akiwa katika ziara ya kikazi leo tarehe 27 Julai 2021. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)

Waziri wa Kilimo Mhe. Prof Adolf Mkenda akikagua ramani ya eneo la kilimo cha Pilipili ambalo lipo chini ya Umoja wa Wajasiriamali wahitimu wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUGECO) kwa ajili ya kilimo cha Pilipili katika kijiji cha Luhindo kilichopo katika Wilaya ya Mvomero, Wakati akiwa katika ziara ya kikazi leo tarehe 27 Julai 2021.
Waziri wa Kilimo Mhe. Prof Adolf Mkenda akijadili jambo na Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mhe Halima Okash pamoja na Mwanzilishi wa SUGECO Dkt Anna Temu mara baada ya kukagua eneo la kilimo cha Pilipili ambalo lipo chini ya Umoja wa Wajasiriamali wahitimu wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUGECO) kwa ajili ya kilimo cha Pilipili katika kijiji cha Luhindo kilichopo katika Wilaya ya Mvomero, Wakati akiwa katika ziara ya kikazi leo tarehe 27 Julai 2021.
Waziri wa Kilimo Mhe. Prof Adolf Mkenda akikagua eneo la kilimo cha Pilipili ambalo lipo chini ya Umoja wa Wajasiriamali wahitimu wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUGECO) kwa ajili ya kilimo cha Pilipili katika kijiji cha Luhindo kilichopo katika Wilaya ya Mvomero, Wakati akiwa katika ziara ya kikazi leo tarehe 27 Julai 2021.
Waziri wa Kilimo Mhe. Prof Adolf Mkenda akizungumza na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Mvomero iliyoongozwa na Mkuu wa wilaya hiyo Mhe Halima Okash kabla ya ziara ya kukagua eneo la kilimo cha Pilipili ambalo lipo chini ya Umoja wa Wajasiriamali wahitimu wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUGECO) kwa ajili ya kilimo cha Pilipili katika kijiji cha Luhindo kilichopo katika Wilaya ya Mvomero, Wakati akiwa katika ziara ya kikazi leo tarehe 27 Julai 2021. 

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Morogoro

Waziri wa Kilimo Mhe. Prof Adolf Mkenda ameielekeza Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kuhakikisha inashirikiana na Umoja wa Wajasiriamali wahitimu wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUGECO) ili kuimarisha miundombinu ya umwagiliaji kwenye shamba la Pilipili mkoani Morogoro.

Waziri Mkenda ametoa maelekezo hayo leo tarehe 27 Julai 2021 wakati alipotembelea na kukagua hatua zilizofikiwa na kusafisha shamba hilo lililopo katika Kijiji cha Luhindo Wilaya ya Mvomero wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja Mkoani Morogoro.

Pia Waziri Mkenda amemuelekeza Mkurugenzi Mtendaji wa Tume hiyo kuhakikisha anashiriki kikamilifu katika usafishaji wa shamba hilo lenye ukubwa wa Hekari 1500 kwa kutumia zana za kisasa ili kumaliza haraka usafishaji wa shamba hilo.

“Ingekuwa ni vizuri tufanye kazi hiyo kwa kasi ili kuweza kulima kwa sehemu kubwa na kuongeza uzalishaji kwa kuwa ardhi ya kutosha ipo, na ajira zinahitajika kwa kiasi kikubwa kwa wananchi hususani vijana ambao ndio nguvu kazi ya Taifa” Amesisitiza Prof Mkenda

Kadhalika amewashukuru wadau wote ikiwemo Benki ya NMB ili kuwezesha upatikanaji wa fedha katika hatua hii ya awali katika kuimarisha miundombi ya kilimo hicho.

Waziri Mkenda amesema kuwa vijana wengi wanaweza kubadilisha mtazamo ikiwa ni pamoja na maisha yao kwa kuingia kwenye kilimo kwani serikali inaendelea kuweka miundombinu rafiki katika sekta ya kilimo.

“Kilimo kinalipa lakini endapo mkulima atakubaliana na mkakati wa kuongeza tija na uzalishaji sasa Kilimo cha Pilipili tayari kina soko na fursa bado ni kubwa kwa vijana kuwekeza kwa wingi” Amekaririwa Prof Mkenda

Waziri wa Kilimo Prof Adolf Mkenda amewaomba wananchi wilayani Mvomero kujitolea mashamba yao ili vijana wengi waweze kujiajiri katika sekta ya kilimo.

Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mhe Halim Okash amesema kuwa mradi huo wa kuendeleza sekta ya kilimo umekuja kwa wakati muafaka kwani suala la ajira kwa vijana limekuwa tatizo kubwa.

    

0 comments:

Post a Comment