Posts

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMANNE JULAI 20, 2021

Image
 

ENDELEENI KUFANYA KAZI KWA UADILIFU NA KUTOA HUDUMA BORA, KM AWAASA WCF

Image
Watumishi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) wameaswa kuendelea kufanya kazi kwa uadilifu na kwa misingi ya uwajibikaji ili kutoa huduma bora kwa wadau wake. Rai hiyo imetolewa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Tixon Nzunda alipotembelea ofisi za Mfuko kwa ajili ya kufuatilia shughuli zinazofanywa na WCF. “Nimefanikiwa kuzungumza na watendaji wa idara na vitengo vyote na moja ya maelekezo yangu ni kuwahimiza kutoa huduma kwa umma kwa kuzingatia misingi ya ueledi, uwajibikaji na usikivu na kuzingatia misingi na miongozo ya uendeshaji kazi serikalini”, alisema Bw. Nzunda. “Pia nawasisitiza kuhakikisha kuwa utendaji wa shughuli za umma unazingatia misingi ya kujenga ustawi wa wananchi. Tumieni rasimilimali zilizopo kwa kuzingatia thamani ya fedha na uwekezaji ufanyike katika maeneo yenye tija ili kulinda amali za fidia kwa wanachama”. Bw. Nzunda ameelekeza Mfuko kuhakikisha unaimarisha zaidi mifumo ya kielekt

DKT. NCHEMBA: SERIKALI IMESIKIA KILIO CHA WANANCHI KUHUSU TOZO ZA MIAMALA YA SIMU

Image
  Naombeni msaada wenu wandugu Na Benny Mwaipaja,Dar es Salaam WAZIRI wa Fedha na Mipango Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amesema Serikali imesikia kilio na maoni ya wananchikuhusu tozo mpya ya miamala ya simu na kuwaomba wawe watulivu wakati jambo hilo linatafutiwa ufumbuzi. Dkt. Nchemba ameyasema hayo Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na vyombo vya habari akiambatana na Waziri wa Teknolojia ha Habari na Mawasiliano Dkt. Faustine Ndugulile. “Kwa maaneo ambayo wananchi wametoa ushauri na kuelezea namna ambavyo jambo hili linawagusa lakini pia tumepokea maeneo ambayo yanatakiwa kutoa elimu zaidi ili kujenga uelewa wa pamoja ikiwa ni pamoja na viwango vinavyokatwa kwa nayetuma na anayetoa lakini pia kuhusu mantiki ya jambo lenyewe” alisema Mhe. Mwigulu Alisema kuwa jambo la tozo za miamala linatekelezwa kupitia sheria iliyopitishwa na Bunge lakini kuna kanuni za utekelezaji zinazo mhusu yeye kama Waziri wa Fedha na Mipango na maeneo mengine yanahusu Wizara ya Teknolloj

Naibu Waziri Gekul amuibua Mbaraka Mwinshekhe mahafali ya Malya

Image
 Adeladius Makwega -Kwimba Mwanza (WHUSM) Serikali imesema kuwa Watanzania wanahitaji burudani ya muziki  kwani  mara baada ya kujishughulisha  na  shughuli  za maendeleo mchana kutwa  basi jioni ni muda wa kupumzisha miili na akili zao. Hayo yamesemwa Julai 17, 2021 katika mahafali ya 10 ya  Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya ambapo Mheshimiwa Pauline Gekul Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo amekuwa mgeni rasmi. “Watanzania tunapenda muziki iwe dansi, Bongo fleva, rege  au  muziki wa kiutamadauni, si mmeona wanachuo cha Malya  walivyokuwa wakicheza muziki  vizuri, huku wakinengua?  huo ndiyo muziki” alisema  Mheshimiwa Gekul. Yawe mashairi au ala za muziki zinaweza kumtoa nyoka pangoni alisema kwa  bashasha huku akiiweka vizuri mikrofoni wakati wa mahafali hayo. Tanzania yetu ina utajiri mkubwa wa muziki mathalani   nyimbo za  zamani zimekuwa  zikipigwa katika  baadhi ya redio na kumbi za starehe. Serikali chini ya Jemedari, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan inatoa ushi

WAZIRI DKT. KALEMANI ASHUSHA UMEME TOKA 3700/- MPAKA 100/- KWA UNIT VISIWANI-MWANZA

Image
 ** Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani Julai 18, 2021 amefanya Ziara katika kisiwa cha Maisome kilichopo wilaya ya Sengerema jijini Mwanza na kuagiza kampuni binafsi ya Jumeme inayosambaza Umeme katika kisiwa hicho kutoza bei elekezi ya Serikali ya Umeme Vijijini ya shilingi 100 kwa unit moja badala ya shilingi 2,000/- mpaka 3,700/- iliyokuwa ikitozwa na kampuni hiyo. Akizungumza na wanakijiji wa kijiji cha Kanoni kisiwani Maisome, Waziri Kalemani alieleza kuwa tayari Serikali imetoa bei elekezi ya umeme nchi nzima ambayo inasimamiwa na EWURA na ndio inayotumika na TANESCO katika kuuzia umeme wananchi hivyo ni vyema wawekezaji wote wakaifuata na kuizingatia. Bei ya kuwauzia umeme wananchi ni moj ambayo inatumika na TANESCO na kusimamiwa na EWURA, hivyo naagiza Kampuni ya Jumeme iwashushie wananchi wa kijiji hichi bei na ifanane na ile inayotozwa na TANESCO katika maeneno mengine na huduma ziboreshwe, umeme usikatike mara kwa mara bila sababu za msingi” Alisema Waziri Kalemani  Wazi

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMATATU JULAI 19, 2021

Image
 

SIMBA YATWAA UBINGWA WA SOKA TANZANIA BARA 2020/2021

Image
Wachezaji wa Simba na benchi la ufundi wakishangilia mara baada ya kutwaa kombe la ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara 2020/2021 baada ya kufikisha pointi 83 kufauatia ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Namungo kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam Julai 18, 2021. Kimainginpambano dhidi ya Namungo lilikuwa la kukamilisha ratiba.