Posts

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMATATU MEI 31, 2021

Image
 

TANESCO YASIFIWA KWA UTEKELEZAJI BORA WA MIRADI.*

Image
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limepongezwa na kusifiwa kwa utekelezaji thabiti wa Miradi mbalimbali ya Umeme ikiwemo miradi mikubwa ya kimkakati na miradi midogo midogo ya usambazaji Umeme Nchini kote.  Pongezi hizo zimetolewa na Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mhe. Anthony Mtaka Tarehe 30 Mei 2021 alipotembelea banda la TANESCO katika maonyesho ya Teknolojia yanayoendelea katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.  Sambamba na pongezi hizo, Mhe Mtaka ameshauri wataalamu wa Tehama wa Shirika kushirikiana na vyuo vya elimu ya juu ili kuboresha mifumo ya utoaji huduma ikiwemo  huduma za ununuzi wa umeme wa LUKU  na kuwezesha wateja kununua umeme kisha umeme huo kuingie  katika mita  bila kumlazimu mteja kwenda kuweka umeme katika mita. Mhe. Mtaka amesema pamoja na mambo mengi mazuri ambayo TANESCO imekuwa ikiyafanya, ni vvyema Shirika likafanya  ushirika na taasisi za elimu ya juu ili kukuza ubunifu na kuwezesha wataalamu wa ndani kutumika katika kutekeleza miradi mbali mbali bila kuhitaji wat

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMAPILI MEI 30, 2021

Image
 

JESHI LA POLISI LIMETOA MAFUNZO KWA MAFUNDI WA MAGARI

Image
  Na Mwandishi Wetu JESHI la Polisi kitengo cha Usalama barabarani, limetoa mafunzo kwa mafundi magari waliyokuwa ndani ya Kituo cha Mabasi cha Magufuli, Mbezi Luis, Dar es Salaam kwa lengo la kuwafundisha jinsi ya kutambua vifaa ambavyo vipo kwenye magari hayo. Mafunzo hayo yametolewa leo Mei 29, 2021 na Mkuu wa Usalama Barabarani, ASP Ibrahim Samwix ,kwa lengo la msfundi hao kutambua mfumo wa injini ya gari unavyofanya kazi ili kuwaraisishia namna ya utengenezaji wa magari. Pia,Mkuu huyo  aliwafundisha kuhusu kifaa cha aina ya turbo kinavyofanya kazi, na namna ya kukitambua kama kikiwa  kibovu, kwa sababu mafundi wengi wamekuwa wakifanya masuala ya ufundi kwa mazoea. ASP Samwix alitoa pia mafunzo katika kifaa cha mfumo wa rejeta namna kinavyofanya kazi, kwa sababu mafundi wengi na madereva wamekuwa wakishindwa kutunza mabasi wanayopewa kutokana na mapungu madogo madogo. Kabla ya mafunzo hayo, Mkuu huyo alianza na madereva kwa kuelimisha jinsi ya kufuata sheria za barabarani na kuende

MKUU WA MAJESHI JENERALI VENANCE MABEYO ATEMBELEA UBALOZI WA TANZANIA- PRETORIA

Image
 Leo Jumamosi tarehe 29 Mei, 2021. Mkuu wa Majeshi wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo, alitembelea Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Afrika Kusini. Jenerali Mabeyo yupo Nchini Afrika Kusini kuhudhuria sherehe za kumuaga Mkuu Majeshi wa Afrika Kusini Jenerali Solly Zacharia Shoke zilizofanyika kitaifa Jana Mjini Pretoria. Kuhudhuria sherehe hizi, ni utaratibu uliowekwa na nchi wanachama wa Jumuiya za SADC ya maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) katika kuimarisha mashirikiano hususan katika Nyanja ya Diplomasia ya Ulinzi (Defence Diplomacy) na Amani katika eneo la nchi za SADC. Jenerali Mabeyo, alikaribishwa Ubalozini na Mhe. Balozi Mej. Jen. Gaudence Salim Milanzi (Mst) na watumishi wa Ubalozi, Mhe. Balozi Milanzi alitoa taarifa fupi ya eneo la uwakilishi ya Afrika Kusini, Botswana na Falme ya Lesotho. Katika taarifa hiyo, Mhe. Balozi alieeza kuwa hali ya uwakilishi inaridhisha kiulinzi na kiusalama, Ubalozi umeendelea kukuza mashirikiano na nchi za e

CHAMA CHA WANASHERIA WANAWAKE (TAWLA) CHAFANYA MKUTANO MKUU WA 31 WA MWAKA

Image
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Tulia Ackson Mwansasu akizungumza katika mkutano wa 31 wa mwaka wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) unaofanyika kwenye Hoteli ya Coral Beach Masaki mkoani Dar es Salaam leo Jumamosi 29,2020. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Tulia Ackson Mwansasu akizungumza katika mkutano wa 31 wa mwaka wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) unaofanyika kwenye Hoteli ya Coral Beach Masaki jijini Dar es Salaam leo Jumamosi 29,2020 Katikati ni  Lulu Ngw'anakilala Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TAWLA na kushoto ni Mwanachama wa TAWLA Flaviana Charles Rwechungura. Balozi Mwanaidi Maajal Mwanachama wa (TAWLA) akiongoza mjadala katika mkutano huo unaofanyika kwenye hoteli ya Coral Beach Masaki jijini Dar es salaam Lulu Ngw'anakilala Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya (TAWLA) akimkaribisha mgeni rasmi ili kuzungumza na wanachama wa taasisi hiyo katika mkutano huo. Naibu

RC KUNENGE AWATAKA VIONGOZI WA HALMASHAURI CHALINZE KUANGALIA VYANZO VINGINE VYA MAPATO

Image
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Abubakar Kunenge amewataka watumishi wa Halmashauri ya Chalinze kuangalia namna ya kubuni vyanzo vingine vya mapato ili kuongeza makusanyo ya Halmashauri hiyo. Kunenge ametoa rai hiyo alipokuwa akiongea na watumishi wa Halmashauri hiyo katika ziara yake ya kujitambulisha kwenye Wilaya ya Bagamoyo mkoani humo. " Siendi kwenye mapato ya jumla naangalia vyanzo maelekezo yangu muangalie namna ya kuongeza vyanzo vingine ili kuongeza makusanyo" alisema Kunenge. Kunenge pia aliongea na Madiwani wa Halmashauri hiyo kusikiliza kero zilizopo kwenye kata zao ili atafute namna ya kuzifanyia kazi baada ya kukamililisha ziara yake kwenye Wilaya na Halmashauri za Mkoa huo. Aliahidi kujenga ushirikiano na wabunge, Madiwani na watumishi ili kufikia lengo la kuwaondolea wananchi kero zinazowakabili. Katika  ziara hiyo Kunenge alipokea madawati 390 kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete ambayo yamelenga kupunguza uhaba wa madawati kwenye shule za Hal