RC KUNENGE AWATAKA VIONGOZI WA HALMASHAURI CHALINZE KUANGALIA VYANZO VINGINE VYA MAPATO

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Abubakar Kunenge amewataka watumishi wa Halmashauri ya Chalinze kuangalia namna ya kubuni vyanzo vingine vya mapato ili kuongeza makusanyo ya Halmashauri hiyo.

Kunenge ametoa rai hiyo alipokuwa akiongea na watumishi wa Halmashauri hiyo katika ziara yake ya kujitambulisha kwenye Wilaya ya Bagamoyo mkoani humo.

" Siendi kwenye mapato ya jumla naangalia vyanzo maelekezo yangu muangalie namna ya kuongeza vyanzo vingine ili kuongeza makusanyo" alisema Kunenge.

Kunenge pia aliongea na Madiwani wa Halmashauri hiyo kusikiliza kero zilizopo kwenye kata zao ili atafute namna ya kuzifanyia kazi baada ya kukamililisha ziara yake kwenye Wilaya na Halmashauri za Mkoa huo.

Aliahidi kujenga ushirikiano na wabunge, Madiwani na watumishi ili kufikia lengo la kuwaondolea wananchi kero zinazowakabili.

Katika  ziara hiyo Kunenge alipokea madawati 390 kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete ambayo yamelenga kupunguza uhaba wa madawati kwenye shule za Halmashauri ya Chalinze.
Alisema, wananchi wanataka mtu wa kuwatatulia kero zao kama alivyofanya Mbunge huyo.



 

Comments

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"