Posts

RC KUNENGE AWATAKA VIONGOZI WA HALMASHAURI CHALINZE KUANGALIA VYANZO VINGINE VYA MAPATO

Image
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Abubakar Kunenge amewataka watumishi wa Halmashauri ya Chalinze kuangalia namna ya kubuni vyanzo vingine vya mapato ili kuongeza makusanyo ya Halmashauri hiyo. Kunenge ametoa rai hiyo alipokuwa akiongea na watumishi wa Halmashauri hiyo katika ziara yake ya kujitambulisha kwenye Wilaya ya Bagamoyo mkoani humo. " Siendi kwenye mapato ya jumla naangalia vyanzo maelekezo yangu muangalie namna ya kuongeza vyanzo vingine ili kuongeza makusanyo" alisema Kunenge. Kunenge pia aliongea na Madiwani wa Halmashauri hiyo kusikiliza kero zilizopo kwenye kata zao ili atafute namna ya kuzifanyia kazi baada ya kukamililisha ziara yake kwenye Wilaya na Halmashauri za Mkoa huo. Aliahidi kujenga ushirikiano na wabunge, Madiwani na watumishi ili kufikia lengo la kuwaondolea wananchi kero zinazowakabili. Katika  ziara hiyo Kunenge alipokea madawati 390 kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete ambayo yamelenga kupunguza uhaba wa madawati kwenye shule za Hal

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMAMOSI MEI 29, 2021

Image
 

RC KUNENGE ATOA ONYO KWA WATENDAJI WA BODI YA MAGHALA NA WAKALA WA VIPIMO

Image
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Abubakar Kunenge ametoa Onyo  kwa watendaji wa Bodi ya Maghala na Wakala wa Vipimo kwa kushindwa kupima mizani zilizopo kwenye  maghala ya Msingi  zinazotumika kupokelea Ufuta na  kushindwa kusimamia maandalizi ya Maghala Makuu, hali inayopelekea kero na kusuasua kwa zao hilo. Ameyasema hayo leo Mei, 26 2021 wakati akiendesha Mkutano wa Wadau wa Ufuta Mkoani hapo, Mkutano huo umefanyika Ikwiriri Wilayani Rufiji. "Natoa Onyo kwa  watendaji wa Serikali siihitaji Ubabaishaji' Changamoto katika zao la  ufuta chanzo pia ni ninyi  Watumishi wa Serikali. Amesema hafurahishwi  na Watendaji hao wa Serikali kusubiri kuitwa na  Wakulima badala ya kuwafuata na kutoa huduma. Ameeleza hatosita kuwaondoa Mkoani hapo kwa kushindwa kusimamia wajibu wao kikamilifu. Aidha, RC Kunenge ametoa siku tatu kwa watendaji hao  kwamba hadi kufikia Mei 28, 2021 kuhakisha kuwa wanakamilisha maandalizi ya Maghala  Makuu na Upimaji wa Mizani kwenye maghala ya Msingi.  

WAZIRI MHAGAMA: TATIZO LA AJIRA NCHINI KUFANYIWA UTAFITI

Image
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu ( Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, akisisitiza umuhimu tafiti za nguvu kazi na Rasilimali watu,  wakati akifungua Kongamano la Wadau wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo  leo tarehe 27 Mei, 2021, Jijini Dodoma.   Katika kuhakikisha malengo ya kutatua masuala ya ajira na kazi, yanafikiwa na Serikali ya Awamu ya Sita inayongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu), imepanga mwaka huu kufanya tafiti mbili kubwa ambazo zitajikita kwenye kubaini nguvu kazi pamoja na rasilimali watu. Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu ( Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, wakati akifungua Kongamano la Wadau wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo  leo tarehe 27 Mei, 2021, Jijini Dodoma. Ameeleza kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi

KUTOKA MAGAZETINI LEO IJUMAA MEI 28, 2021

Image