RC KUNENGE ATOA ONYO KWA WATENDAJI WA BODI YA MAGHALA NA WAKALA WA VIPIMO
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Abubakar Kunenge ametoa Onyo kwa watendaji wa Bodi ya Maghala na Wakala wa Vipimo kwa kushindwa kupima mizani zilizopo kwenye maghala ya Msingi zinazotumika kupokelea Ufuta na kushindwa kusimamia maandalizi ya Maghala Makuu, hali inayopelekea kero na kusuasua kwa zao hilo.
Ameyasema hayo leo Mei, 26 2021 wakati akiendesha Mkutano wa Wadau wa Ufuta Mkoani hapo, Mkutano huo umefanyika Ikwiriri Wilayani Rufiji.
"Natoa Onyo kwa watendaji wa Serikali siihitaji Ubabaishaji' Changamoto katika zao la ufuta chanzo pia ni ninyi Watumishi wa Serikali.
Amesema hafurahishwi na Watendaji hao wa Serikali kusubiri kuitwa na Wakulima badala ya kuwafuata na kutoa huduma. Ameeleza hatosita kuwaondoa Mkoani hapo kwa kushindwa kusimamia wajibu wao kikamilifu.
Aidha, RC Kunenge ametoa siku tatu kwa watendaji hao kwamba hadi kufikia Mei 28, 2021 kuhakisha kuwa wanakamilisha maandalizi ya Maghala Makuu na Upimaji wa Mizani kwenye maghala ya Msingi.
Comments
Post a Comment