Posts

RAIS SAMIA AKUTANA NA RAIS MSTAAFU WA NIGERIA OLESEGUN OBASANJO IKULU CHAMWINO

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na mgeni wake Rais (mstaafu) wa Nigeria Mhe. Olesegun Obasanjo mara baada ya mazungumzo yao Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma Aprili 3, 2021 . Mazungumzo hayo pia yalihudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Liberata Mulamula. (PICHA NA IKULU)  

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMATATU MEI 3, 2021

Image
 

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMAPILI MEI 2, 2021

Image
 

RAIS SAMIA AHUTUBIA WAFANYAKAZI KILELE CHA MEI MOSI JIJINI MWANZA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwahutubia Wafanyakazi mbalimbali katika Kilele cha Sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi Kitaifa ambazo zimefanyika Jijini Mwanza leo tarehe 01 Mei, 2021 katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza  

WAFANYAKAZI TANESCO WASHIRIKI MAANDAMANO YA MEI MOSI KITAIFA JIJINI MWANZA

Image
WAFANYAKAZI wa Shirika la Umeme Nchini TANESCO wameungana na  Wafanyakazi wenzao kutoka Sekta ya Umma na Binafsi katika maandamano ya siku ya Wafanyakazi Duniani maarufu Mei Mosi kitaifa jijini Mwanza Mei 1, 2021. Msafara wa maandamano hayo ulipokelewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Mhe. Samia Suluhu Hassan katika uwanja wa CCM Kirumba jijini mwanza ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni “Maslahi Bora, Mishahara Juu, Kazi Iendelee”. Maandamano hayo ya wafanyakazi yalifuatiwa na misafara ya magari ya taasisi mbalimbali za Umma na Binafsi yakionyesha kazi zinazotekelezwa na taasisi hizo. Rais Samia anatarajiwa kuwahutubia wafanyakazi katika sherehe hizo ambazo ni za kwanza kuhutubiwa na kiongozi huyo wa Serikali ya Awamu ya Sita. Wafanyakazi wa Shirika la Umeme Nchini TANESCO, wakijumuika na wafanyakazi wengine katika maandamano ya sherehe za MEI MOSI Kitaifa jijini Mwanza leo asubuhi.