WAFANYAKAZI TANESCO WASHIRIKI MAANDAMANO YA MEI MOSI KITAIFA JIJINI MWANZA

WAFANYAKAZI wa Shirika la Umeme Nchini TANESCO wameungana na  Wafanyakazi wenzao kutoka Sekta ya Umma na Binafsi katika maandamano ya siku ya Wafanyakazi Duniani maarufu Mei Mosi kitaifa jijini Mwanza Mei 1, 2021.

Msafara wa maandamano hayo ulipokelewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Mhe. Samia Suluhu Hassan katika uwanja wa CCM Kirumba jijini mwanza ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni “Maslahi Bora, Mishahara Juu, Kazi Iendelee”.

Maandamano hayo ya wafanyakazi yalifuatiwa na misafara ya magari ya taasisi mbalimbali za Umma na Binafsi yakionyesha kazi zinazotekelezwa na taasisi hizo.

Rais Samia anatarajiwa kuwahutubia wafanyakazi katika sherehe hizo ambazo ni za kwanza kuhutubiwa na kiongozi huyo wa Serikali ya Awamu ya Sita.

Wafanyakazi wa Shirika la Umeme Nchini TANESCO, wakijumuika na wafanyakazi wengine katika maandamano ya sherehe za MEI MOSI Kitaifa jijini Mwanza leo asubuhi.






 

Comments

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"