DARAJA LA KIYEGEYA MBIONI KUKAMILIKA
Meneja wa TANROADS, mkoa wa Morogoro, Mhandisi, Kolante Ntije, akimuonesha Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi, Dkt. Leonard Chamuriho (mwenye tai), mihimili mikuu itakayowekwa kwenye daraja la Kiyegeya, mkoani Morogoro, wakati Waziri huyo alipofika darajani hapo kujionea maendeleo yake. Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi, Dkt. Leonard Chamuriho (mwenye tai), akiangalia mihimili mikuu itakayowekwa kwenye daraja la Kiyegeya, mkoani Morogoro, wakati Waziri huyo alipofika darajani hapo kujionea maendeleo yake. Muonekano wa mihimili mikuu itayowekwa katika daraja la Kiyegeya ikiwa imekamilika. Muonekano wa moja ya nguzo zitakazoshikilia daraja la Kiyegeya ikiwa katika hatua za mwisho kukamilika.PICHA NA WUU Serikali imesema inatarajia kukamilisha ujenzi wa daraja la Kiyegeya, mkoani Morogoro, hivi karibuni, ambalo lilibomoka mwezi Machi, mwaka jana kutokana na mvua kubwa zilizokuwa zikinyesha. Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja hi