KILIMO HAI NI AJIRA YA UHAKIKA KWA VIJANA

Afisa Tathmini na Ufuatiliaji wa SAT Yohana Haule akiwa amemshika mkono Mtaribu wa Mradi wa Kilimo Hai wilaya ya Mlimba Elizabeth Msobi jana wakivuka mto kwenda kukagua mashamba ya vijana wakati wa ziara ya wataalam wa Wizara ya Kilimo kutembelea vikundi vya vijana kijiji cha Kalengakelu wilaya ya Mlimba.

Afisa Tathmini na Ufuatiliaji wa SAT Yohana Haule akiwa amemshika mkono Mtaribu wa Mradi wa Kilimo Hai wilaya ya Mlimba Elizabeth Msobi jana wakivuka mto kwenda kukagua mashamba ya vijana wakati wa ziara ya wataalam wa Wizara ya Kilimo kutembelea vikundi vya vijana kijiji cha Kalengakelu wilaya ya Mlimba.(Picha na Wizara ya Kilimo)

Mratibu wa Mkakati wa Vijana kushiriki kwenye kilimo toka Wizara ya Kilimo Revelian Ngaiza (kushoto aliyevaa tshirt blu) akiongea na Afisa Mtathmini wa shirika la SAT wakiwa kwenye shamba la mpunga lililolimwa na vijana kwa nia ya kilimo hai jana kijiji cha Kalengakelu wilaya ya Mlimba. SAT inatekeleza mkakati huo kwa kuwaunganisha vijana na kuwapa elimu ya kilimo hai pamoja na ujasiliamali .
Picha ya pamoja ya wataalam wa Wizara ya Kilimo pamoja na vijana wa kikundi cha Kilimo Hai kijiji ch Kalengakelu wilaya ya Mlimba waliojiunga pamoja kuzalisha kujiajili kwenye kilimo ikiwa ni utekelezaji wa Mkakati wa Vijana Kushiriki kwenye Kilimo wa mwaka 2016.
Lucia Mussa mwanachama wa kikundi cha Kilimo Hai kijiji cha Kalengakelu wilaya ya Mlimba akielezea namna ya kuzalisha mazao ya bustani kwa njia ya kilimo hai jana alipotembelewa na wataalam wa wizara ya kilimo. Ametoa ombi kwa serikali kusaidia upatikanaji wa madawa ya asili kuua wadudu hususan wakati wa mvua .
Mratibu wa Mkakati wa Vijana kushiriki katika kilimo toka Wizara ya Kilimo Revelian Ngaiza (kushoto) akiongea na mratibu wa kikundi cha vijana wilaya ya Mlimba wanaolima kilimo hai  Elizabeth Msobi (kulia) jana walipotembelea shamba la mpunga kijiji cha Kalengakelu wilaya ya Mlimba .
 

Vijana nchini wameshauriwa kujiunga katika vikundi na kuanzisha mashamba yanayotumia kilimo hai kwa kulima bila kutumia kemikali ili kuwa na uhakika wa soko na kipato.
Kauli hiyo imetolewa na Mratibu wa Mkakati wa Vijana Kushiriki katika kilimo toka Wizara ya Kilimo Revelian Ngaiza jana (27.04.2021) wakati alipotembelea vikundi vya vijana wanaofanya kazi za kilimo hai kijiji cha Kalengakelu wilaya ya Mlimba Mkoa wa Morogoro.
Ngaiza aliongozana na wataalam wa shirika la Kilimo Endelevu (Sustainable Agriculture of Tanzania-SAT) alijionea mashamba ya mpunga ya vijana wa kijiji cha Kalengaleku ikiwemo vitongoji vya Nyumbanguru na Samola ambao wanazalisha mazao ya mpunga na mazao ya bustani kwa njia ya kilimo hai.
"Lengo la Wizara ya Kilimo ni kuona nguvu kazi iliyopo ya vijana takribani asilimia 58 inashiriki kwenye kazi za uzalishaji mali kupitia kilimo ili kukuza uchumi wa kaya na taifa" alisema Ngaiza.
Mratibu huyo wa Mkakati wa Vijana katika kilimo alibainisha fursa zilizopo kwenye kilimo ikiwemo kilimo hai ambacho hakitumii kemikali kuwa ni uhakika wa masoko kutokana na watum wengi kupenda kutumia vyakula vilivyozalishwa bila kemikali 
Naye Mratibu wa mradi wa Kilimo Hai toka shirika la SAT  wilaya ya Mlimba Elizabeth Msobi alisema jumla ya vijana 97 kwenye kijiji cha Kalengakelu wamejiunga kwenye vikundi na wanazalisha mazao ya mpunga na bustani kwa njia ya kilimo hai (organic farming) bila kutumia kemikali au madawa kuua wadudu hivyo kutunza mazaingira na afya ya mlaji.
Msobi aliongeza kusema changamoto kubwa kwa vijanwa Mlimba ni ukosefu wa ardhi hali inayokatisha tamaa vijana wengi kujiunga hususan wanawake  .
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kikundi cha Kilimo Hai Kitongoji cha Samola kijiji cha Kalengakelu Daud  Kalinga aliomba serikali iagize viongozi wa vijiji kugawa ardhi kwa vijana.
"Serikali itupatie ardhi sisi vijana ili tulime Kilimo hai badala ya sasa tunachangishana kukodi ekari moja kwa shilingi 100,000 ni fedha nyingi mno,tunashindwa kufanya kilimo" alisema kijana Daudi.

Comments

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"