Posts

KILIMO HAI NI AJIRA YA UHAKIKA KWA VIJANA

Image
Afisa Tathmini na Ufuatiliaji wa SAT Yohana Haule akiwa amemshika mkono Mtaribu wa Mradi wa Kilimo Hai wilaya ya Mlimba Elizabeth Msobi jana wakivuka mto kwenda kukagua mashamba ya vijana wakati wa ziara ya wataalam wa Wizara ya Kilimo kutembelea vikundi vya vijana kijiji cha Kalengakelu wilaya ya Mlimba. Afisa Tathmini na Ufuatiliaji wa SAT Yohana Haule akiwa amemshika mkono Mtaribu wa Mradi wa Kilimo Hai wilaya ya Mlimba Elizabeth Msobi jana wakivuka mto kwenda kukagua mashamba ya vijana wakati wa ziara ya wataalam wa Wizara ya Kilimo kutembelea vikundi vya vijana kijiji cha Kalengakelu wilaya ya Mlimba.(Picha na Wizara ya Kilimo) Mratibu wa Mkakati wa Vijana kushiriki kwenye kilimo toka Wizara ya Kilimo Revelian Ngaiza (kushoto aliyevaa tshirt blu) akiongea na Afisa Mtathmini wa shirika la SAT wakiwa kwenye shamba la mpunga lililolimwa na vijana kwa nia ya kilimo hai jana kijiji cha Kalengakelu wilaya ya Mlimba. SAT inatekeleza mkakati huo kwa kuwaunganisha vijana na kuwapa elimu ya

MJUMBE WA KAMATI KUU YA CCM, RAIS SAMIA AUNGANA NA WAJUMBE WENZAKE KWENYE KIKAO KINACHOFANYIKA DODOMA

Image
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM, na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan na wajumbe wengine wakiwa tayari kuanza kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho kinachoongozwa na Makamu Mwenyekiti wake (bara) Ndugu Philip Mangula akisaidiana na Makamu wa Mwenyekiti mwenza (Visiwani) Rais Mstaafu wa Zanzibar Ali Mohamed Shein katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre jijini Dodoma leo Jumatano Aprili 28, 2021.  

AWESO ATOA SIKU 10 MRADI WA MAJI MWAKITOLYO SHINYANGA UKAMILIKE

Image
Waziri wa Maji Jumaa Aweso, (katikati mwenye shati la bluu) akiwa kwenye ziara ya kukagua mradi wa Maji Mwakitolyo wilayani Shinyanga, wa tatu kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko.

TBS YATOA ELIMU KWA WASINDIKAJI, WAJASIRIAMALI NA WADAU WA MCHELE KAHAMA

Image
  Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limetoa elimu kwa wasindikaji, wajasiriamali na wadau wa mchele wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga katika mnyororo wa thamani kuhusu kanuni bora za uzalishaji,matakwa ya viwango,namna bora ya uhifadhi,elimu juu ya vifungashio na taarifa za msingi zinazotakiwa kuwepo kwenye vifungashio. Mafunzo hayo yamefanyika leo Jumanne Aprili 27,2021 katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama na kukutanisha wajasiriamali 100 wanaojihusisha na bidhaa ya Mchele ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha. Akifungua mafunzo hayo, Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha aliishukuru TBS kwa kukutana na wasindikaji, wajasiriamali na wadau wa mchele akieleza kuwa ni kundi la wajasiriamali ambao ni sehemu muhimu katika sekta binafsi inayochangia pato la taifa,kuongeza ajira na kuondoa umaskini nchini.  “Wilaya ya Kahama ni moja ya wilaya za kimkakati katika uwekezaji mkubwa katika sekta y

RAIS WA ZANZIBAR DKT. HUSSEIN ALI MWINYI AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA UFARANSA NCHINI TANZANIA IKULU

Image
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akisalimiania na Balozi wa Ufaransa Nchini Tanzania Mhe.Frederic Clavier kwa kugonganisha mikoni alipowasili katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha leo 27-4-2021.(Picha na Ikulu) RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Balozi wa Ufaransa Nchini Tanzania Mhe. Frederic Clavier (kulia kwa Rais) akiwa na ujumbe wake, alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha, mazungumzo yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.leo 27-4-2021.(Picha na Ikulu) RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Balozi wa Ufaransa Nchini Tanzania Mhe. Frederic Clavier, alipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha, mazungumzo hayo yamefanyika katika ukumbiu wa Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu) RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hus

HUDUMA YA MAMA NA MTOTO YATAKIWA KUWEPO KATIKA NGAZI ZOTE ZA UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA NCHINI

Image
  Na.Catherine Sungura,WAMJW-Morogoro Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima ameagiza majengo yote ya vituo vya kutolea Huduma ambayo bado hayajaanza kutoa Huduma za afya kote nchini kuanza Mara moja kutoa Huduma za mama na mtoto ikiwemo utoaji wa chanjo ili kupunguza changamoto za afya. Dkt. Gwajima ameyasema hayo leo mkoni Morogoro wakati akifungua maadhimisho ya wiki ya chanjo ambayo Kitaifa yamefanyika Kwenye viwanja vya Chamwino. Dkt. Gwajima amesema kuwa yapo majengo mengi yamejengwa lakini hayajaanza kutoa huduma za Magonjwa ya nje (OPD) na kuagiza yaanze Sasa kutoa huduma za mama na mtoto ikiwemo Chanjo ili kuwapunguzia mwendo mrefu akina mama wajawazito na Watoto. Kwa upande wa maadhimisho ya wiki ya Chanjo Dkt. Gwajima amesema madhumuni ya wiki hii ni kuhamasisha na kuelimisha Jamii kuhusu umuhimu wa huduma za Chanjo Katika kukinga Magonjwa yanayozuilika kwa Chanjo na kuepusha vifo vinavyoweza kuzuilika kwa Chanjo. "Ninawahimiza