WAZIRI MHAGAMA ATATUA KERO ZA WAFANYAKAZI KATIKA SHAMBA LA MKONGE LA KIGOMBE ESTATE
Na Mwandishi Wetu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama ametatua kero na changamoto zilizokuwa zikiwakabili wafanyakazi wa Shamba la Mkonge la Kigombe Estate, Wilayani Muheza dhidi ya mwajiri wao kufuatia malalamiko ambayo yaliwasilishwa wakati wa ziara ya Waziri Mkuu. Akizungumza wakati wa ziara yake hiyo ya kikazi ambayo ilikuwa imelenga utekelezaji wa Maagizo ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa aliyoyatoa tarehe 21 Januari, 2021 alipotembelea shamba hilo la Mkonge lililopo chini ya kampuni ya Amboni Plantation Limited. Mara baada ya kusikiliza pande zote mbili Waziri Mhagama alieleza kuwa kutokana na malalamiko mbalimbali yaliyowasilishwa na wafanyakazi inadhihirisha kuwepo na mapungufu makubwa katika utekelezaji wa sheria za kazi ambazo zimechangia kwa kiasi kikubwa migogoro kutokea. “Mwajiri anawajibu wa kusikiliza kero na malalamiko ya wafanyakazi wali