WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI NAO WAJIONEA KWA MACHO KASI YA UJENZI MRADI WA UMEME WA MAJI WA JNHPP 2115
NA
K-VIS BLOG, JNHPP RUFIJI
WAHARIRI wa vyombo vya habari wametembelea mradi mkubwa wa kimkakati wa bwawa la kufua umeme wa
maji la Julius Nyerere (JNHPP-2115) lililoko bonde la mto Rufiji na kujionea ujenzi
ukiendelea kwa kasi katika maeneo yote muhimu matano.
Wakiongozwa
na Mhandisi wa Bwawa, Mhandisi Kamugenyi Luteganya Februari 28, 2021 wahariri
hao walitembeela eneo la ujenzi wa bwawa (Main Dam), eneo la kuchepusha maji (Diversion tunnel), eneo
la power intake na eneo la kufua
umeme (Power generation).
Lakini
pia waandishi hao walitembelea maeneo mengine ya ujenzi kama vile eneo la
kuchukulia umeme (Switch Yard) na sehemu ya mitambo ya kuchanganya zege.
Mapema
akizungumza na wahariri hao katika kikao kazi baina ya TANESCO ambao ndio
wasimamizi wa mradi kwa niaba ya serikali na wahariri mjini Morogoro Februari
27, 2021, Waziri wa Nishati Dk. Medard Kalemani aliwahakikishia kuwa ujenzi
utakamilika kama ambavyo mkataba unavyosema Juni 2022.
“Napenda niwahakikishie kuwa ujenzi eneo la
mradi unaendelea usiku na mchana na kuongeza mradi huu ambao unafadhiliwa
kwa asilimia 100 na Serikali kwa thamani ya Shilingi Trilioni 6.5 ni wa kwanza
kwa ukubwa katika nchi za Afrika Mashariki na wanne kwa ukumbwa barani Afrika,
utaleta manufaa makubwa siyo tu ya kuzalisha umeme Megawati 2115 bali pia utunzaji
wa mazingira, kilimo cha umwagiliaji na ufugaji.
Comments
Post a Comment