Posts

MAONYESHO YA BIASHARA NA TEKNOLOJIA YA MADINI YAZINDULIWA SHINYANGA

Image
  Mgeni Rasmi mkuu wa mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel, akizungumza kwenye maonyesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini mkoani Shinyanga. Eneo la maonyesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini mkoani Shinyanga, lililopo eneo la Butulwa Kata ya Old -Shinyanga. Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, akisoma taarifa kwenye maonyesho hayo ya Biashara na Teknolojia ya Madini. Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi, akisoma taarifa ya maonyesho hayo ya Biashara na Teknolojia ya Madini. Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini Patrobas Katambi, akizungumza kwenye maonyesho hayo ya Biashara na Teknolojia ya Madini mkoani Shinyanga. Mwenyekiti wa Chemba ya wafanyabiashara na viwanda mkoani Shinyanga Meshack Kulwa, akitoa shukrani kwenye maonyesho hayo ya Biashara na Teknolojia ya Madini. Mkuu wa mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel, (wa tatu kutoka kulia) akizindua maonyesho ya Biashara na Teknolojia ya madini mkoani Shinyanga, wapili kulia ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zain

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMAPILI NOVEMBA 29, 2020

Image
 

WAZIRI MKUU MAJALIWA AWA MBOGO, AMWAMBIA MKURUGENZI AKAE PEMBENI KWA KUDHARAU MAAGIZO YA SERIKALI

Image
  WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Karibu Mkuu wizara ya KILIMO kumuondoa kwenye nafasi take MKURUGENZI wa Bodi ya maghala Bw. Odilo  Majengo kwa kushindwa kutekeleza maagizo ya Serikali kuhusu kusitisha tozo ya unyaufu katika zao la korosho. Waziri Mkuu ametoa agizo Hilo wakati wa kikao chake na Wakuu wa Mikoa ya Pwani, Lindi, Mtwara na Ruvuma, Makatibu Wakuu wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Kilimo, Viwanda na Biashara pamoja Mrajisi wa Ushirika. Kikao hicho kimefanyika kwenye  ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa  jijini Dodoma  Novemba 28, 2020. Pia Waziri Mkuu amewaagiza waendesha maghala kuacha kukata tozo ya upungufu wa uzito wa korosho ghafi zilizohifadhiwa ghalani (unyaufu) kwa wakulima na wanunuzi kwa kuwa TOZO hiyo imeshaondolewa na suala hilo halijathibitishwa kitaalamu. “Mimi niliwaita kuwaambia kuwa wasimamizi wa maghala hampaswi kukata tozo ya unyaufu iwe ni kwa wakulima au wanunuzi kwasababu tozo hii haina uhalisia na haijathibitishwa na na

DKT. MPANGO AHIMIZA KILIMO CHA KISASA KIGOMA

Image
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akisalimiana na Mkazi wa Kijiji cha Kilelema, wilayani Buhigwe, Kigoma, Bw. Benedicto Joseph, wakati wa ziara yake ya kikazi katika Kata ya Kilelema, wilayani Buhigwe mkoani Kigoma. Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akiagana na wakazi wa Kata ya Kilelema, baada ya kuwashukuru kwa kumchagua kwa kishindo Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na yeye binafsi kwa kura za kishindo wakati wa Uchaguzi Mkuu uliomalizika hivi karibuni. (Picha na Josephine Majura -KIGOMA)   Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akizungumza na wananchi wa Kata ya Kilelema Wilayani Buhigwe mkoani Kigoma, alipofanya ziara ya kuwashukuru kwa kumchagua kuwa Mbunge wa Jimbo hilo.   Baadhi ya wakazi wa Kata ya Kilelema, Wilayani Buhigwe mkoani Kigoma, wakimsikiliza Waziri wa Fedha na Mipango na Mbunge wa Jimbo la Buhigwe Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, (Hayupo pichani),

MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM JIJINI DODOMA

Image
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein pamoja na Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi wakati wakitoka kwenye Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM kilichofanyika jijini Dodoma leo tarehe 28 Novemba 2020. Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi wakati wakiimba Wimbo wa Chama pamoja na Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM muda mfupi kabla ya kuanza kuongoza kikao hicho leo tarehe 28 Novemba, 2020 jijini Dodoma  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM mkoani Dodoma leo tarehe 28 jijini Dodoma. (Picha na IKULU).