WAZIRI MKUU MAJALIWA AWA MBOGO, AMWAMBIA MKURUGENZI AKAE PEMBENI KWA KUDHARAU MAAGIZO YA SERIKALI

 
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa 

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Karibu Mkuu wizara ya KILIMO kumuondoa kwenye nafasi take MKURUGENZI wa Bodi ya maghala Bw. Odilo Majengo kwa kushindwa kutekeleza maagizo ya Serikali kuhusu kusitisha tozo ya unyaufu katika zao la korosho.

Waziri Mkuu ametoa agizo Hilo wakati wa kikao chake na Wakuu wa Mikoa ya Pwani, Lindi, Mtwara na Ruvuma, Makatibu Wakuu wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Kilimo, Viwanda na Biashara pamoja Mrajisi wa Ushirika. Kikao hicho kimefanyika kwenye  ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa  jijini Dodoma  Novemba 28, 2020.

Pia Waziri Mkuu amewaagiza waendesha maghala kuacha kukata tozo ya upungufu wa uzito wa korosho ghafi zilizohifadhiwa ghalani (unyaufu) kwa wakulima na wanunuzi kwa kuwa TOZO hiyo imeshaondolewa na suala hilo halijathibitishwa kitaalamu.

“Mimi niliwaita kuwaambia kuwa wasimamizi wa maghala hampaswi kukata tozo ya unyaufu iwe ni kwa wakulima au wanunuzi kwasababu tozo hii haina uhalisia na haijathibitishwa na na vyombo husika, hakuna unyaufu unaotokea katika kipindi kifupi cha kuhifadhi korosho, hayo yote ni mawazo yenu tu”,”Amesema.





Comments

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"