Posts

WAZIRI MKUU MAJALIWA AWA MBOGO, AMWAMBIA MKURUGENZI AKAE PEMBENI KWA KUDHARAU MAAGIZO YA SERIKALI

Image
  WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Karibu Mkuu wizara ya KILIMO kumuondoa kwenye nafasi take MKURUGENZI wa Bodi ya maghala Bw. Odilo  Majengo kwa kushindwa kutekeleza maagizo ya Serikali kuhusu kusitisha tozo ya unyaufu katika zao la korosho. Waziri Mkuu ametoa agizo Hilo wakati wa kikao chake na Wakuu wa Mikoa ya Pwani, Lindi, Mtwara na Ruvuma, Makatibu Wakuu wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Kilimo, Viwanda na Biashara pamoja Mrajisi wa Ushirika. Kikao hicho kimefanyika kwenye  ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa  jijini Dodoma  Novemba 28, 2020. Pia Waziri Mkuu amewaagiza waendesha maghala kuacha kukata tozo ya upungufu wa uzito wa korosho ghafi zilizohifadhiwa ghalani (unyaufu) kwa wakulima na wanunuzi kwa kuwa TOZO hiyo imeshaondolewa na suala hilo halijathibitishwa kitaalamu. “Mimi niliwaita kuwaambia kuwa wasimamizi wa maghala hampaswi kukata tozo ya unyaufu iwe ni kwa wakulima au wanunuzi kwasababu tozo hii haina uhalisia na haijathibitishwa na na

DKT. MPANGO AHIMIZA KILIMO CHA KISASA KIGOMA

Image
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akisalimiana na Mkazi wa Kijiji cha Kilelema, wilayani Buhigwe, Kigoma, Bw. Benedicto Joseph, wakati wa ziara yake ya kikazi katika Kata ya Kilelema, wilayani Buhigwe mkoani Kigoma. Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akiagana na wakazi wa Kata ya Kilelema, baada ya kuwashukuru kwa kumchagua kwa kishindo Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na yeye binafsi kwa kura za kishindo wakati wa Uchaguzi Mkuu uliomalizika hivi karibuni. (Picha na Josephine Majura -KIGOMA)   Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akizungumza na wananchi wa Kata ya Kilelema Wilayani Buhigwe mkoani Kigoma, alipofanya ziara ya kuwashukuru kwa kumchagua kuwa Mbunge wa Jimbo hilo.   Baadhi ya wakazi wa Kata ya Kilelema, Wilayani Buhigwe mkoani Kigoma, wakimsikiliza Waziri wa Fedha na Mipango na Mbunge wa Jimbo la Buhigwe Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, (Hayupo pichani),

MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM JIJINI DODOMA

Image
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein pamoja na Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi wakati wakitoka kwenye Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM kilichofanyika jijini Dodoma leo tarehe 28 Novemba 2020. Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi wakati wakiimba Wimbo wa Chama pamoja na Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM muda mfupi kabla ya kuanza kuongoza kikao hicho leo tarehe 28 Novemba, 2020 jijini Dodoma  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM mkoani Dodoma leo tarehe 28 jijini Dodoma. (Picha na IKULU).

Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Habari Lajionea Ujenzi wa SGR

Image
Na Shamimu Nyaki -WHUSM, Morogoro.   Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi  wa  Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  wa metembelea  M radi wa  K imkakati wa Reli ya Kisasa (SGR) kipande cha Morogoro - Dodoma ambapo wamefurahishwa na namna mradi huo unavyotekelezwa kwa kasi. Akizungumza kwa niaba ya baraza hilo ,  Novemba 27, 2020 Mkuu wa msafara ambaye  ni Mkurugenzi  wa  Idara ya Sera na Mipango, Bw. Petro Lyatuu ,  amesema kwamba ziara hiyo imekuwa na manufaa kwa kuwa wajumbe wa baraza wamejifunza kwa vitendo namna mradi unavyotekelezwa hatua kwa hatua. "Tumekua na siku nzuri leo tumejifunza kwa kuona jinsi Serikali inavyotekeleza mradi huu, tumeona hatua il i yofikiwa katika ujenzi ikiwemo usimikwaji wa nguzo za umeme pamoja na utandikaji wa mataruma ya reli, naamini tutakua mabalozi wazuri katika kuelimisha na kushawishi wengine waje wajifunze na kuona kazi inayofanyika hapa" amesema Bw. Lyatuu. Kwa upande wake Mhandisi Msaidizi wa Mradi kutoka Shirika la Reli Tanzan

TARURA YADHAMIRIA KUUNGANISHA WILAYA YA RUANGWA NA LIWALE

Image
N a Bebi Kapenya   Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), umeendelea kuboresha miundombinu ya barabara na madaraja katika Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Mkoa wa Lindi ikiwemo ujenzi wa daraja la Mto Mbwemkuru lenye urefu wa mita 75  linalojengwa katika barabara ya Chikwale hadi Liwale  kwa gharama ya Shilingi Bilioni 4.5. Meneja wa TARURA Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Mhandisi Mashaka Nalupi alisema mradi wa ujenzi wa daraja la Mto Mbwemkuru umetokana na mpango wa kuunganisha Wilaya ya Ruangwa na Wilaya ya Liwale kwa lengo la kurahisisha mawasiliano kwa wananchi wa maeneo hayo na kuwezesha shughuli zao za kiuchumi na kijamii kwa haraka. “ Wilaya hizi mbili ni maarufu sana katika kilimo cha korosho na ufuta, lakini pia wananchi wa vijiji vya Nangurugai, Mirui, Narungombe, Machang’anja na Chikwale watapata faida ya kiuchumi kwasababu mazao yao ya biashara yataweza kuvushwa kutoka upande wa Liwale kwenda Ruangwa ambapo kuna soko kubwa la mazao ya biashara pale Ruangwa mj

KAMATI YA USALAMA WILAYA YA IKUNGI SINGIDA YAKAGUA MIRADI YA ELIMU NA AFYA

Image
  Wajumbe wa Kamati ya Usalama ya Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, wakijadiliana wakati wa ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya Elimu na Afya wilayani humo. Kamati hiyo iliongozwa na Mwenyekiti wake Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo. Moja ya chumba cha darasa kilicho kaguliwa na kamati hiyo. Baadhi ya madarasa yaliyokaguliwa. Muonekano wa vyoo vya Shule ya Msingi vilivyo kaguliwa na kamati hiyo. Muonekano wa baadhi ya madarasa yaliyokaguliwa na kamati hiyo. Muonekano wa baadhi ya madarasa yaliyokaguliwa na kamati hiyo. Ukaguzi ukiendelea.  Wajumbe wa kamati hiyo wakikagua ujenzi wa Chuo cha Veta. Kushoto mbele ni  Mwenyekiti wa kamati hiyo Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo. Muonekano wa ndani wa baadhi ya madarasa ya shule za sekondari yaliyokaguliwa na kamati hiyo. Muonekano wa ndani wa baadhi ya madarasa ya shule za sekondari yaliyokaguliwa na kamati hiyo. Moja ya chumba cha darasa cha shule ya sekondari kilicho kaguliwa na kamati hiyo. Jengo la Maabara lililokaguliwa

MTATURU AANZA KUTEKELEZA AHADI ZA WANANCHI KWA KASI YA 4G

Image
  Wachungaji na waumini wa  Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT)  Usharika wa Kiaskofu Msalaba Mrefu mjini Singida, wakiwa na pikipiki walizokabidhiwa hivi karibuni na Mbunge  wa Singida Mashariki, Miraji Mtaturu kwa ajili ya kazi za kanisa hilo, Mbunge  wa Singida Mashariki, Miraji Mtaturu, akimkabidhi pikipiki, Mkuu wa Jimbo la Kusini Usharika wa Issuna, Mchungaji, Obedi Msele. Mbunge  wa Singida Mashariki, Miraji Mtaturu, akimkabidhi pikipiki, Mchungaji Joyce Madadi wa Usharika wa Ikungi.   Mbunge  wa Singida Mashariki, Miraji Mtaturu, akimkabidhi pikipiki, Mchungaji, Felix Kibiriti. Na Dotto Mwaibale, Singida. MBUNGE wa Singida Mashariki, Miraji Mtaturu ameanza kutekeleza ahadi zake kwa wananchi kwa kasi ya 4G. Mtaturu ametekeleza ahadi yake  kwa kutoa pikipiki tano kwa Usharika wa Kiaskofu Msalaba Mrefu mjini Singida ambazo alimkabidhi Mchungaji Felix Kibiriti kwa niaba ya Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kati Dkt. Alex Mkumbo kwa aj