Posts

MAANDALIZI YA KUMPOKEA MGOMBEA URAIS WA CCM MKOANI SINGIDA YANAENDELEA

Image
Katibu wa Siasa na Uenezi wa  Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa  wa Singida Ahmed Kaburu, akionesha l lani ya  Chama cha Mapinduzi (CCM)   ya mwaka 2020-2025 wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya  kumpokea mgombea Urais wa chama hicho Dkt.John Magufuli ambaye anatarajia kuwasili mkoani hapa kesho. Mabango yenye picha za mgombea huyo yakiwekwa Barabara Kuu ya Singida Dodoma.   Watoto Ashiruna Athumani (kushoto) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la pili Shule ya Msingi Utemini mkoani hapa  na wadogo zake wakitazama picha ya mgombea huyo iliyoweka viwanja vya Bombadia. Vijana wa Jeshi la Akiba wakisafisha eneo la uwanja utakapofanyika mkutano wa mgombea huyo. Uwanja utakapofanyika mkutano huo. Mabango yenye picha za mgombea huyo yakiwa yamewekwa Barabara Kuu ya Singida Dodoma.   Mafundi wakiendelea na kazi ya kusimika Jukwaa utakapofanyika mkutano huo.    Mafundi wakiendelea na kazi ya kusimika Jukwaa utakapofanyika mkutano huo. Wajasiriamali wakichangamkia fursa ya mku

MWAKALINGA ATETA NA WATUMISHI WA TAASISI ZA SEKTA YA UJENZI

Image
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga, akitoa maelekezo kwa Kaimu Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), mkoa wa Shinyanga Daniel Ojwando, wakati Katibu Mkuu huyo alipokuwa akikagua Karakana ya TEMESA mkoani humo. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga, akisisitiza jambo kwa watumishi wa Taasisi zilizo chini ya Sekta yake (hawapo pichani) alipokutana nao mkoani Shinyanga kujadili masuala mbalimbali ya kiutumishi. Watumishi wa Taasisi zilizo chini ya Sekta ya Ujenzi, wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga (hayupo pichani) wakati alipokutana nao kujadili masuala mbalimbali ya kiutumishi.   Mfanyakazi kutoka Wakala wa Barabara (TANROADS) mkoa wa Shinyanga, Gryson Lwiza, akitoa maoni yake wakati Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Arch. Elius Mwakali

HESLB YAONGEZA MUDA WA KUPOKEA MAOMBI YA MIKOPO YA WANAFUNZI ELIMU YA JUU

Image
ISMAIL NGAYONGA, DAR ES SALAAM BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imeamua kuongeza muda wa kupokea maombi ya mikopo kutoka kwa wanafunzi hadi Septemba 10, 2020 mwaka huu, Mkurugenzi Mtendaji Abdul-Razaq Badru amesema. Bw. Badru ameyasema hayo wakati akitoa taarifa kwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. James Mdoe leo (Jumatatu, Agosti 31, 2020) amefalipofika kwenye ofisi za Bodi hiyo jijini Dar es Salaam kwa nia ya kujionea utendaji kazi wa Bodi. “Tunaendelea vizuri na majukumu yetu na kutokana na   kupokea maoni mengi ya wadau, HESLB imeamua kuongeza muda wa kupokea maombi ya mikopo kutoka kwa wanafunzi hadi Septemba 10 mwaka huu.” Alisema. Bw. Abdul-Razak Badru alisema  “Mwisho ilikua iwe leo saa sita usiku, lakini tumeamua kuongeza siku kumi ili kuwawezesha wateja wetu ambao hawajakamilisha maombi yao kufanya hivyo,” amesema Badru na kuongeza kuwa uamuzi huo umefuatia mashauriano na wadau wengine kama Wakala wa Usajili, Ufilisi n

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMANNE SEPTEMBA 1, 2020

Image
 

TCRA, UCSAF WAKUTANA NA WADAU WA MAWASILIANO KANDA YA ZIWA….WASISITIZA KUJENGA MINARA YA PAMOJA

Image
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) akifungua Mkutano wa wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa. Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kushirikiana na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) umekutana na wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa wakiwemo wamiliki wa vituo vya Radio, Televisheni, watoa huduma za usafirishaji wa vifurushi na watoa huduma ya maudhui mtandaoni kwa lengo la kuwajengea uelewa watoa huduma na wadau hao kushiriki shughuli za mfuko wa UCSAF na kutimiza wajibu wao kisheria.  Akizungumza katika Mkutano huo leo Agosti,31 2020 uliofanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mkuu wa Idara ya Fedha na Utawala UCSAF, Pius Joseph alisema mkutano ulilenga kuwajengea uelewa wadau wa mawasiliano namna mfuko wa UCSAF unavyofanya kazi na wajibu wao kisheria. Joseph aliyataja miongoni mwa mafani

MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM RAIS MHE. DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM JIJINI DODOMA

Image
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM, Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi pamoja na Wajumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM wakati wakiimba Wimbo wa Chama kabla ya kuongoza Kikao hicho cha Kamati Kuu jijini Dodoma leo tarehe 31 Agosti 2020  

KATIBU MKUU KILIMO GERALD KUSAYA AJADILI NAMNA YA KUINUA KILIMO CHA MBOGA NA MATUNDA (HORTICULTURE), ARUSHA

Image
KATIBU Mkuu Wizara ya Kilimo, Bw. Gerald Kusaya (pichani kushoto) amefanya kikao na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Kuendeleza Mazao ya Bustani (TAHA) Dkt.Jacquline  Mkindi jijini Arusha cha kujadili mikakati na mambo mbalimbali yahusuyo maendeleo ya tasnia ya mboga mboga na matunda (horticulture) nchini.   Sambamba na kikao hicho, Katibu Mkuu Kusaya ameikabidhi TAHA zawadi ya Ramani ya Tanzania inayoonesha viwango vya pH na Afya ya Udongo kwa nchi nzima na imepokelewa na Mtendaji Mkuu wa TAHA, Dr. Jacqueline Mkindi. Kusaya ameitaka TAHA kuendelea kuelimisha wakulima wengi zaidi kuzingatia kilimo cha kitaalam kwa kutambua aina ya udongo unaofaa kwa zao husika na mbolea gani itumike, ndio maana amekabidhi ramani hiyo kuwezesha utambuzi wa maeneo yanayofaa kwa mazao ya horticulture nchini. "Tunaendelea kuishukuru Serikali kupitia Wizara ya Kilimo kwa ushirikiano mkubwa na wa muda wote inaotupatia wadau wa sekta ya horticulture " Dr Mkindi alisema. Katibu Mkuu Kusaya alikuwa mkoani