Tuesday, September 1, 2020

MWAKALINGA ATETA NA WATUMISHI WA TAASISI ZA SEKTA YA UJENZI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga, akitoa maelekezo kwa Kaimu Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), mkoa wa Shinyanga Daniel Ojwando, wakati Katibu Mkuu huyo alipokuwa akikagua Karakana ya TEMESA mkoani humo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga, akisisitiza jambo kwa watumishi wa Taasisi zilizo chini ya Sekta yake (hawapo pichani) alipokutana nao mkoani Shinyanga kujadili masuala mbalimbali ya kiutumishi.

Watumishi wa Taasisi zilizo chini ya Sekta ya Ujenzi, wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga (hayupo pichani) wakati alipokutana nao kujadili masuala mbalimbali ya kiutumishi.


 Mfanyakazi kutoka Wakala wa Barabara (TANROADS) mkoa wa Shinyanga, Gryson Lwiza, akitoa maoni yake wakati Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga,  alipokutana na watumishi wa Taasisi zilizo chini ya Sekta yake kujadili masuala mbalimbali ya kiutumishi.

0 comments:

Post a Comment