HESLB YAONGEZA MUDA WA KUPOKEA MAOMBI YA MIKOPO YA WANAFUNZI ELIMU YA JUU

ISMAIL NGAYONGA, DAR ES SALAAM

BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imeamua kuongeza muda wa kupokea maombi ya mikopo kutoka kwa wanafunzi hadi Septemba 10, 2020 mwaka huu, Mkurugenzi Mtendaji Abdul-Razaq Badru amesema.

Bw. Badru ameyasema hayo wakati akitoa taarifa kwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. James Mdoe leo (Jumatatu, Agosti 31, 2020) amefalipofika kwenye ofisi za Bodi hiyo jijini Dar es Salaam kwa nia ya kujionea utendaji kazi wa Bodi.

“Tunaendelea vizuri na majukumu yetu na kutokana na   kupokea maoni mengi ya wadau, HESLB imeamua kuongeza muda wa kupokea maombi ya mikopo kutoka kwa wanafunzi hadi Septemba 10 mwaka huu.” Alisema.

Bw. Abdul-Razak Badru alisema  “Mwisho ilikua iwe leo saa sita usiku, lakini tumeamua kuongeza siku kumi ili kuwawezesha wateja wetu ambao hawajakamilisha maombi yao kufanya hivyo,” amesema Badru na kuongeza kuwa uamuzi huo umefuatia mashauriano na wadau wengine kama Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) na Shirika la Posta Tanzania (TPC) ambazo nazo zinawahudumia wateja hao.

Kuhusu malipo kwa wanafunzi waliopo vyuoni, Badru amesema TZS 15.57 bilioni zimetumwa vyuoni kwa ajili ya kuwawezesha wanafunzi wanufaika 39,721 kuendelea na mafunzo kwa vitendo katika maeneo mbalimbali kuanzia wiki hii.

 Kwa upande wake, Prof. Mdoe aliieleza  Menejimenti hiyo ya HESLB chini ya Mkurugenzi Mtendaji Abdul-Razaq Badru kuwa waendelee kuchapa kazi.

“Nimekuja kuona mmejiandaaje na mwaka mpya wa masomo na hali ya uombaji mikopo inavyoendelea na nimefurahi kusikia mnaendelea vizuri, endeleeni kuchapa kazi,” amesema Prof. Mdoe katika kikao kazi na wajumbe wa menejimenti ya HESLB kilichofanyika katika ofisi za HESLB zilizopo eneo la TAZARA.

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimuya Juu (HESLB) Abdul-Razaq Badru (kushoto) akifafanua jambo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe wakati alipofanya ziara katika Ofisi za HESLB na kuzungumza na menejimenti ya HESLB iliyoongozwa na Mkurugenzi Mtendaji leo Jumatatu (Agosti 31, 2020) Jijini Dar es Salaam.


 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. James Mdoe (kulia) akimsikiliza Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe wakati wa ziara yake ya kikazi katika Ofisi za HESLB ambapo alizungumza na menejimenti ya HESLB iliyoongozwa na Mkurugenzi Mtendaji leo Jumatatu (Agosti 31, 2020). Kushoto ni Mkuu wa MawasilianO HESLB, Omega Ngole.(PICHA NA BODI YA MIKOPO- HESLB)

 

Comments

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"