Posts

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMAPILI AGOSTI 30, 2020

Image
 

CCM YAZINDUA KAMPENI KWA KISHINDO

Image
Mgombea kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, akihutubia maelfu ya wananchi waliofurika ndani na nje ya uwanja wa michezo wa Jamhuri jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa kampeni za Chama hicho leo Agosti 29, 2020. (PICHA NA IKULU)   Mgombea wa Urais kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi wa Dodoma wakati wa uzinduzi wa Kampeni za CCM kwa upande wa Urais, Wabunge na Madiwani katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. (PICHA NA IKULU) Mgombea wa Urais kwa Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akicheza pamoja na Wanamuziki wa Bendi ya TOT mara baada ya kuwasili katika uwanja wa mpira wa Jamhuri jijini Dodoma kwa ajili ya uzinduzi wa Kampeni za CCM.  (PICHA NA IKULU)     Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Abdul Naseeb kwa jina la Diamond Platnumz akifanya vitu vyake wakati wa uzinduzi

CCM WANA JAMBO LAO UWANJA WA JAMHURI JIJINI DODOMA LEO.

Image
NA SAID MWISHEHE,MICHUZI TV CHAMA Cha Mapinduzi(CCM)kimesema kesho Agosti 29 mwaka huu wa 2020 wana jambo lao ambalo ni la uzinduzi rasmi wa Kampeni za Mgombea wa Urais wa Chama hicho Dk.John Magufuli huku kikieleza kitatumia nafasi hiyo kuielezea Afrika na Dunia mambo makubwa yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ga Tano. Akizungumza leo Agosti 28,2020, katika Uwanja Jamhuri jijini Dodoma ,Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Humphrey Polepole amefafanua maandalizi yote kuelekea uzinduzi wa kampeni za mgombea Urais na ratiba itaanza saa moja asubuhi hadi saa 12 jioni.   "Watanzania na wana CCM kesho hapa uwanja wa Jamhuri tuna jambo letu tunawakaribisha wote.Kesho tunataka kuisimamisha Tanzania,Afrika na Dunia kwa kuelezea mafanikio ambayo yamepatika katika kipindi cha miaka mitano chini ya jemedari wetu Dk.John Magufuli,"amesema Polepole na kusisitiza watu watafurika uwanjani hapo kuanzia saa 12 asubuhi. Amesema kwamba baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC)

KATIBU MKUU KILIMO ATEMBEELA KIWANDA CHA KUZALISHA MBOLEA CHA MINJINGU MKOANI MANYARA

Image
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya (kulia) akiongea na viongozi wa kiwanda cha mbolea cha Minjingu cha Manyara leo alipowatembelea kukagua uzalishaji.Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda hicho Bw.Tosky Hans Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha mbolea cha Minjingi Bw.Tosky Hans leo alipowasili kiwandani hapo mkoani Manyara kwa ziara ya kukagua hali ya uzalishaji mbolea. Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya (kushoto ) akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa kiwanda cha Kahela Feeders cha Arusha Bw.Alex Kahela ( kulia) kuhakikisha anasajili bidhaa zake kwenye mamlaka za ubora ili zitambulike kwenye soko .(Picha na habari Wizara ya Kilimo) Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya akiwa ameshika chupa ya mbolea ya maji (Booster) inayozalishwa na kiwanda cha Keen Feeders cha Arusha leo alipotembelea.Akiwa kiwandani hapo ameagiza bidhaa zote hizo zisajiliwe na kupata nembo ya ubora kabla hazijaingizwa sokoni ili kuml