WANANCHI WAFURIKA BANDA LA JKCI, MAONESHO YA OSHA ARUSHA
NA
K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, ARUSHA
WANANCHI
kutoka maeneo mbalimbali ya jiji la Arusha, wamejitokeza kwa wingi kwenye banda
la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI),
ili kupata huduma za kitabibu kwenye Maonesho ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi
(OSHA) katika viwanja vya General Tyre,
Njiro jijini Arusha.
Miongoni
mwa huduma zitolewazo na wataalamu wa JKCI wakiongozwa na Daktari Bingwa wa
Magonjwa ya Moyo, JKCI, Dkt. Dickson Minja ni uchunguzi wa magonjwa yote ya
moyo na mishipa ya damu ikiwemo upimaji wa msukumo wa damu (blood pressure),
upimaji wa sukari, Echo, Uzito, BMI na urefu.
Aidha
wanaanchi wanaofika kwenye banda hilo pia wanapatiwa ushauri wa kitabibu kutoka
kwa Daktari huyo Bingwa, Dkt. Dickson Minja.
Huduma
zote hizo za uchunguzi zinatoelwa bure.
Benson
Bisare, Afisa Muuguzi JKCI, akimuhudumia mwananchi huyu kwa kumpima Blood Pressure
(BP) kwenye banda la Taasisi hiyo kwenye viwanja vya General Tyre, Njiro,
jijini Arusha, Aprili 27, 2024.
Odilia Njau, Afisa Muuguzi JKCI, akimuhudumia mwananchi huyu wakati anapima urefu (Weight) na uzito (BMI).
Comments
Post a Comment