RAIS MWINYI KATIKA SHEREHE ZA MIAKA 60 YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Zanzibar itaendelea kuwa muumini wa dhati wa Muungano kwa kuudumisha na kuuimarisha kwa faida ya kizazi cha sasa na vijavyo. \n\nRais Dk.Mwinyi akizungumza katika kilele cha Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yalioongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam tarehe 26 , Aprili 2024.\n\nAidha Rais Dk.Mwinyi amesema Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Imeendelea kupata sifa na heshima kubwa kimataifa kwa kuwa nchi ya mfano kwa kudumu kwa Muungano wa kuwa na amani , umoja na mshikamano .\n\nHalikadhalika Rais Dk.Mwinyi amesema Tanzania imepata mafanikio makubwa yaliyotokana na Muungano katika sekta mbalimbali kiuchumi na huduma za kijamii.\n\nKwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi amewashukuru Viongozi wa awamu zilizopita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa jitihada za kudumisha na kuendeleza malengo ya Tanzania na kuzifanyia kazi changamoto zinazojitokeza na kuzifanyia ufumbuzi.









Comments

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"