KAMISHNA GENERALI WA DAWA ZA KULEVYA AIPONGEZA OFISI YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI

  

Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Aretas Lyimo (Kulia) akimsikiliza Mkurugenzi wa Huduma za Sayansi jinai David Elias kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali aliyekua akimpa maelezo wakati Kamishna huyo alipitembelea Banda la Mkemia Mkuu katika maonesho ya Wiki ya Sheria Kitaifa yanayofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma. 
Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Aretas Lyimo (kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi wa Huduma za Sayansi jinai David Elias kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali aliyekua akimpa maelezo wakati Kamishna huyo alipitembelea Banda la Mkemia Mkuu katika maonesho ya Wiki ya Sheria Kitaifa yanayofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma. 


Na Sylvester omary, Dodoma
Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Aretas Lyimo, ameipongeza Mamlaka ya Maabara ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa utoaji wa haraka wa ripoti za uchunguzi na uboreshaji wa mifumo ya utendaji kazi.
Kamishna Jenerali ameyasema hayo leo jijini Dodoma alipotembelea banda la Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwenye maadhimisho ya Wiki ya Sheria yanayofanyika katika viwanja vya Nyerere Square. 
“Nawapongeza kwa kuwahisha ripoti za uchunguzi na kuendana na kasi ya Serikali ya awamu ya sita kwa kununua mitambo imara na yenye ubora katika uchunguzi wa kimaabara na kupata ithibati za mifumo ya kimataifa” alisema Kamishna Jenerali.
Aidha, Kamishna Aretas Lyimo, alipongeza Mamlaka kwa kuwa na mifumo ya taarifa za uchunguzi wa kimaabara na wa taarifa za mashahidi wataalam ambayo inasaidia kubadilisha taarifa na wadau wengine wa haki jinai. 
 “Nawapongeza pia kwa kuwa na mifumo ya kufanyia kazi ya kisasa, hii yote inasaidia kuongeza utendaji kazi na kusaidia vyombo vingine na Mahakama kwenye utendaji haki ili kuleta ustawi kwa Taifa” alisema.

Comments

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"