MAONESHO YA MADINI GEITA: NAIBU GAVANA BOT DKT. YAMUNGU KAYANDAMBILA ATEMBELEA BANDA LA PSSSF
Naibu
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dkt. Yamungu Kayandabila (anayezungumza
pichani kulia), ametembelea banda la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa
Umma, (PSSSF), kwenye Maonesho ya 6 ya Teknolojia ya Madini, kwenye viwanja vya
EPZA, Bombambili mjini Geita.
Akiwa katika banda hilo, Dkt. Kayandabila, ambaye alifuatana na
Meneja Uhusuano BoT, Bi. Vicky Msina, alipokelewa na Meneja wa PSSSF,
Kanda ya Magharibi, Bw. Geofrey Kolongo.
Bw. Kolongo alimueleza huduma zilizotolewa na PSSSF kwa wananchi
na wanachama wa PSSSF ambao ni watumishi wa umma, waliotembeela banda hilo
ambapo alisema, wanachama waliweza kupatiwa taarifa kuhusu uanachama wao ikiwa ni
pamoja na kupata taarifa za Michango, taarifa za Mafao yatolewayo na Mfuko,
wastaafu waliweza kujihakiki kwa kutumia alama za vidole lakini pia
walielimishwa jinsi ya kutumia huduma ya PSSSF kiganjani, ambayo inamuwezesha
mwanachama na mwajiri kupata taarifa na huduma mbalimbali za Mfuko.
Pia wanachama na wananchi walipatiwa taarifa ya uwekezaji
unaotekelezwa na Mfuko, kwenye maeneo mbalimbali.
Maonesho hayo yalizinduliwa Septemba 26, 2023 na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Doto Bitekoyamebeba kauli mbiu; Matumizi ya teknolojia sahihi katika kuinua wachimbaji wadogo kiuchumi na kuhifadhi mazingira yamewaleta pamoja washiriki zaidi ya 400 na yanatarajiwa kufikia kilele Septemba 30, 2023
Comments
Post a Comment