TANAPA YAKUBALI KUANZISHA KITUO KIDOGO CHA ASKARI WA UHIFADHI KATA YA KIHANGA - KARAGWE KUDHIBITI UVAMIZI WA TEMBO.

 Karagwe - Kagera.

Mbunge wa Jimbo la Karagwe, Innocent Bashungwa amefikia makubaliano na Shirika la Hifadhi ya Taifa Tanzania - TANAPA kuanzisha kituo Kidogo cha askari wa uhifadhi katika kata ya Kihanga wilaya Karagwe ili kudhibiti uharibifu unaofanywa na tembo na wanyama wengine wakali wanaoshambulia Wananchi na mali zao mara kwa mara.

Makubaliano hayo yamefikiwa leo tarehe 30, Januari 2023 wakati Bashungwa akisikiliza na kutatua kero za wananchi katika Mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Kibwera kata ya Kihanga wilaya ya Karagwe.

Bashungwa ameitaka Halmashauri ya wilaya Karagwe kushirikiana na TANAPA kutoa elimu kwa jamii na kuuunda Vikundi vitakavyokuwa vinashirikana na askari wa Uhifadhi watakaokaa katika kata hiyo kwa ajili ya kulinda usalama wa wananchi na mali zao.

Amemtaka Kamishina Msaidizi wa TANAPA Kanda ya ziwa kukamilisha taratibu wa Kulipa fidia kwa wananchi kata Kihanga ambao wameharibiwa mali zao kwa kuvamiwa na tembo ili waweze kupatiwa kifuta machozi kulingana na taratibu za Serikali.

Kwa upande wake, Kamishina Msaidizi wa TANAPA Kanda ya Ziwa, John Antony Nyamuhanga amewahakikishia wananchi kuwa  kuanzia leo kutakuwa na askari wa uhifadhi na gari katika Kata ya Kihanga kuhakikisha hakuna uharibifu wa wanyama unaoendelea kufanyika katika kata ya kihanga na maeneo jirani.

Kadhalika, Bashungwa wakati akiongea na wananchi amesema huduma za afya katika kata Kihanga zinaendelea kuboresha ambapo katika Kata hiyo zipo Zahanati mbili za Kishoju na Kibwera ambazo sasa zimejengewa mahabara na zinatoa huduma ya Ultrasound.

Katika Sekta ya Elimu, Bashungwa ameeleza kuwa kata ya Kihanga imekuwa na muamko mkubwa wa elimu ndiyo maana hata Shule ya Wasichana Maalum ya Sayansi ya Mkoa wa Kagera inaendelea kujengwa katika kata hiyo.

Pia, Bashungwa amesema TARURA itaendelea kutenga fedha kukarabari barabara ya Kihanga Kwenda Mshabaiguru mpaka Kigarama iendelee kupitika vizuri misimu yote ili wananchi waweze kusafirisha mazao yao kirahisi.












Comments

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"