WAZIRI JENISTA AIASA TUME YA UTUMISHI WA UMMA KUSIMAMIA HAKI WAKATI WA KUTOA MAAMUZI YA MASHAURI YA KINIDHAMU
Na Veronica
Mwafisi, Dodoma
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.
Jenista Mhagama ameiasa Tume ya Utumishi wa Umma kusimamia haki wakati wa kutoa
maamuzi ya mashauri ya kinidhamu ya watumishi wa umma yaliyowasilishwa ili
kutolewa maamuzi.
Mhe.
Jenista ametoa nasaha hizo jijini Dodoma wakati wa kikao kazi chake na Makamishna
wa Tume ya Utumishi wa Umma, kilichofanyika ofisini kwake kwa lengo la kuhimiza
uwajibikaji katika Tume ya Utumishi wa Umma.
Mhe.
Jenista ameitaka Tume ya Utumishi wa Umma kutoa maamuzi ya mashauri yote ya
kinidhamu kwa kuzingatia haki, kwa mujibu wa Sheria, Kanuni, Taratibu na
Miongozo ya Utumishi wa Umma iliyopo.
Waziri
Jenista ameongeza kuwa, Tume isipo yashughulikia mashauri ya kinidhamu kwa haki
na wakati, inakwamisha maendeleo ya nchi yasipatikane kwa wakati na ndio maana
Serikali imekuwa ikiihimiza Tume ya Utumishi wa Umma kutekeleza wajibu wao kwa
wakati na kwa kutenda haki.
“Jambo
la msingi hakikisheni haki inatendeka katika mashauri ya kinidhamu, mkifanya
hivyo mtakuwa mnasimamia na kujenga nidhamu nzuri ya utendaji kazi katika
Utumishi wa Umma,” Mhe. Jenista amesisitiza.
Aidha,
Mhe. Jenista amezungumzia changamoto ukiukwaji wa Sheria, Kanuni, Taratibu na
Miongozo ya utumishi wa umma unaofanywa
na baadhi ya waajiri na watumishi, hivyo amewataka Makamishna wa Tume ya
Utumishi wa Umma kufanyia kazi changamoto hiyo.
Akizungumza
kwa niaba ya Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma, Mhe. Balozi John Haule amemshukuru Mhe. Jenista
Mhagama kwa kuwahimiza kutenda haki wakati wa kushughulikia mashauri ya
kinidhamu na kumuahidi kuwa watatoa maamuzi ya mashauri ya kinidhamu kwa mujibu
wa Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo iliyopo katika Utumishi wa Umma.
Tume
ya Utumishi wa Umma imeundwa chini ya kifungu Na. 9 (1) cha Sheria ya Utumishi
wa Umma, Sura ya 298. Tume hii ina jukumu la kufuatilia na kusimamia uendeshaji
wa shughuli za rasilimaliwatu katika Taasisi za Umma ikiwa ni pamoja na
kuhakikisha Utumishi wa umma unaendeshwa kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na
Taratibu.
Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Jenista Mhagama (meza kuu katikati) wakati akizungumza nao kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akitoa neno la utangulizi kabla ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Jenista Mhagama kuzungumza na Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma, Mhe. Jaji (Mst.) Hamisa Kalombola akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Tume ya Utumishi wa Umma kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Jenista Mhagama kabla ya Waziri huyo kuzungumza na Makamishna wa Tume hiyo kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.
Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma, Mhe. Balozi John Haule akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Jenista Mhagama mara baada ya Waziri huyo kuzungumza nao kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.
Comments
Post a Comment