NGULI WA MASUALA YA UCHUMI PROFESA HONEST NGOWI AFARIKI KATIKA AJALI YA BARABARANI


 NGULI wa masuala ya Uchumi nchini, Prpofesa Honest Ngowi (pichani juu) amefariki dunia katika ajali ya gari mapema asubuhi hii ya Machi 28, 2022.

Habari zilizopatikana mapema leo zinasema Profesa Ngowi ambaye alikuwa ni Mchumi mbobezi akifanya kazi katika Chuo Kikuu cha Mzumbe mkoani Morogoro, amefariki yeye na dereva wake papo hapo, baada ya gari walilokuwa wakisafiria kuangukiwa na Kontena maeneo ya Mlandizi mkoani Pwani.

Taarifa fupi kutoka idara ya Mawasiliano ya Chuo Kikuu cha Mzumbe imesema "Habari Wote. Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Lughano Kusiluka anasikitika kutangaza kifo cha Prof. Honest Ngowi na Dereva wake, waliofariki asubuhi ya leo kwa ajali ya gari wakiwa njiani kuja Kampasi Kuu Morogoro. Tunaomba muwe watulivu wakati Menejiementi inaendelea kufuatilia taarifa kamili ya tukio hili, na kuweka taratibu zingine. Taarifa zaidi  zitatolewa rasmi na taratibu zingine za kuwahifadhi wenzetu. Bwana alitoa na Bwana Ametwaa jina la Bwana lihimidiwe. Poleni Wote kwa msiba huu mzito." Taarifa hiyi ilisema.



Comments

  1. Poleni sana familia ya prof Ngowi n.a. jamii ya chuo kikuu cha mzumbe kwa ujumla!
    Hakika Tanzania imepoteza kumbe!!

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"