BOTI YAZAMA PEMBA, MIILI 9 YAOPOLEWA, 15 WANUSURIKA NA WENGINE BADO HAWAJULIKANI WALIPO

 Na MWANDISHI wetu.

WATU Tisa (9) wamefariki baada ya boti waliokuwa wakisafiria kuzama baharini kisiwani Pemba, Kamanda wa Polisi mkoa wa Kusini Pemba, Kamishna Msaidizi wa  Polisi (ACP) Richard Tadei amethibitisha.

ACP Tadei amesema boti hiyo iliyokuwa na abiria zaidi ya 30 ilikuwa ikisafiri kutoka Chakechake kuelekea kisiwa kidogo cha Panza kilichoko mkoa wa Kusini Pemba Januari 4, 2022.

"Watu hawa walikuwa wanaelekea msibani na katika hatua ya awali ya uokoaji tumefanikiwa kupata miili 9, na watu 15 wakiwa hai". Alisema ACP Tadei.

Hata hivyo hakuaema chanzo Cha ajali hiyo ni nini hasa.

Alisema Kazi ya uokoaji iliyokuwa ikiongozwa na vyombo vya ulinzi na Usalama kwa kushirikiana na wananchi imeahirishwa kwa muda kutokana na hali mbaya ya hewa na inatarajiwa kuendelea tena leo.

Alisema Miili ya waliofariki imehifadhiwa kwenye Hospitali ya Mkoani ya Abdallah Mzee kwa ajli ya uchunguzi wa kitabibu na baada ya hapo wananchi wataruhusiwa kutambua wapendwa wao kwa ajili ya mazishi.



Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"