BALOZI MASHIBA AWATOA HOFU MADEREVA WA TANZANIA HUKO MALAWI

 Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Mhe. Benedict Mashiba amewatoa hofu Watanzania kuwa Madereva wa Malori wa Tanzania wapo salama licha ya kulengwa na wenzao wa Malawi.

Kwa mujibu wa Balozi Mashiba, visa vya kushambuliwa kwa Malori yanayoe deshwa na Madereva wa Tanzania nchini Malawi vilianza Jumatatu Septemba 27, 2021 ambapo Madereva wa Malori wa Nchini Malawi waliitisha mgomo wakidai maslahi Bora kutoka kwa waajiri wao.

Taarifa za vyombo vya habari zikinukuu vyanzo mbalimbali kutoka nchini Malawi vilisema, Madereva wa Malawi waliamuru Malori yote ya mizigo kuegeshwa na yasiobekane barabarani Hadi hapo madai yao yatakapopatiwa ufumbuzi. 

Hata hivyo Madereva wa Malori kutoka Tanzania hawakujihusisha na mgomo huo kwasababu hakuwa ukiwahusu na waliendelea na kazi Hali iliyowakasitisha wenzao na hivyo kuyashambulia Malori yao kwa mawe na kuharibu vioo.

 Balozi Mashiba jana Septemba 29, 2021 alikutana na baadhi ya Madereva wa Tanzania na kushauriana nao kuhusu namna Bora ya kuepuka mashambulizi hayo.

Aidha Polisi nchini Malawi wametoa idhini Madereva wa Tanzania waendelee na safari zao. 

" Sisi Ubalozini tunafuatilia hatua zinazochukuliwa na serikali kuhakikisha usalama wa watu wetu kupitia Wizara yao ya Mambo ya Nje." Alisema Balozi Mashiba.

Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Mhe. Benedict Mashiba (katikati mwenye suti) akiwa katika picha na baadhi ya Madereva wa Tanzania waliokumbwa na msukosuko huko Malawi.

Comments

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"