WEKEZENI KWENYE MIRADI AMBAYO HAITAWASUMBUA; MKURUGENZI MKUU PSSSF, CPA HOSEA KASHIMBA
NA MWANDISHI WETU
MKURUGENZI
Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), CPA. Hosea
Kashimba amewaasa wastaafu watarajiwa kuwekeza kwenye miradi ambayo haitawasumbua
pindi watakapokuwa nje ya utumishi wa Umma.
CPA.
Kashimba ametoa rai hiyo leo Agosti 5, 2021, wakati akifunga mafunzo ya Awamu ya
Kwanza ya Semina kwa wastaafu watarajiwa kwa mwaka wa fedha 2021/2022 jijini
Dar es Salaam.
“Tunawaomba
sana muwekeze katika mambo ambayo hayatawasumbua kama mlivyofundishwa katika
semina hii…mfannye vitu ambavyo mnavifahamu.”Alisema.
Alitoa
mfano wa Mstaafu mmoja ambaye yeye baada ya kulipwa mafao yake alienda kununua
daladala 10 ili afanye biashara ya usafirishaji na kwakuwa hakuwa na uzoefu
wowote wa biashara hiyo haikudumu na biashara hiyo “ikafa”.
“
Kwa hiyo tuangalie kama ni kuanza biashara za daladala ni vema ukaanza mapema
ukiwa bado uko kwenye utumishi na usisubiri kustaafu halafu ndiyo uanze biashara
ya daladala, itakusumbua sana,”alisema.
Alisema
ni matumaini yake semina hiyo imewasaidia sana wastaafu hao kujua namna gani wanapaswa
kuishi wakiwa nje ya utumishi wa umma na kuwaandaa kufanya matumizi sahihi ya
fedha watakazolipwa ili waendelee kuishi maisha ya furaha na amani.
Washiriki wa semina hiyo iliyowaleta pamoja watumishi wa umma wa
kada mbalimbali jijini Dar es Salaam ambao wanatarajia kustaafu katika vipindi
tofauti ambapo wapo waliobakiza miaka mitano wastaafu, wengine mitatu, miwili
na mmoja.
Katika awamu hii ya kwanza semina hizo zimeshafanyika kwenye mikoa
mbalimbali zikianza Julai 14, 2021 jijini Dodoma, na kuendelea kwenye mikoa ya
Mwanza, Mbeya, Tanga, Arusha, Ruvuma, Mtwara, Morogoro, Zanzibar na kumalizia
na Dar es Salaam.
Akitoa maoni yake baada ya mafunzo hayo, Bi.Doroth ambaye ni mstaafu
mtarajiwa yeye amefurahishwa na elimu kuhusu kuwekeza katika hati fungani na
kwa elimu aliyoipata hatababaika wapi awekeze fedha zake.
Amewaasa wenzake wanaotarajiwa kustaafu kujihadhari na matapeli
kwani wana namna nyingi za hadaa na pindi wanapopata taarifa kutoka kwa mtu
ambaye haeleweki watoe taarifa kwenye vyombo vya dola.
“Tujiepushe na watu tusiowafahamu na hata wale tunaowafahamu kwani
itasaidia kupoteza fedha utakazolipwa.” Alisema.
Comments
Post a Comment